Je ni vitu vipi hivyo viwili vya Mungu visivyoweza kubadilika? (Waebrania 6:18)

Je ni vitu vipi hivyo viwili vya Mungu visivyoweza kubadilika? (Waebrania 6:18)

SWALI: Tukisoma Kitabu cha Waebrania tunaona mwandishi akitaja vitu viwili vya Mungu visivyoweza Kubadilika ambavyo tumepewa viwe kama nanga ya Roho, je ni vipi hivyo? Au Maana yake ni nini?

Waebrania 6:17-19

[17]Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;

[18]ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;

[19]tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,


JIBU: Ukisoma hiyo habari vifungu vya juu na vile vinavyoendelea mbele yake. Habari inayozungumziwa pale ni ya Ibrahimu na jinsi Mungu alivyompa ahadi ya mbaraka pamoja na uzao wake. Na jinsi alivyokuja kuitimiza

Lakini tunaonyeshwa ahadi ile pekee aliyopewa, haikutosha kumfanya Ibrahimu, aamini bali Mungu Ili kumthibitishia kuwa atavipokea kweli kweli basi aliongezea Na kiapo.

Mwanzo 22:15-17

[15]Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni

[16]akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

[17]katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

Kwasababu kiapo ni kifungo cha mwisho ambacho Mtu humaliza shuku zote, mashaka yote mijadala yote..

Ilimbidi Mungu aweke kiapo ijapokuwa angetimiza Ahadi zake bila kiapo. Lakini ilimbidi afanye vile ili kumpa uthabiti Ibrahimu juu ya maadhimio yake.

Hivyo mambo hayo mawili yasiyoweza Kubadilika ya Mungu ni;

1)Neno lake(ambalo lilikuja kama ahadi),

2) lakini pia Kiapo, ambacho hukata maneno yote.

Na kweli tunakuja kuona yote Mungu aliyomuahidi Ibrahimu yalitokea kama yalivyo..

Lakini Ahadi hiyo haikuishia kwa Ibrahimu, bali ilitimilizwa yote na Bwana wetu Yesu Kristo.

Ambao sisi tuliomwamini, tunaingizwa Katika ahadi hizo..alizozithibitisha Kwa kiapo kupitia Bwana wetu Yesu Kristo. Ambaye Mungu alimthibitisha kama kuhani mkuu wa milele mfano wa Melkizedeki kuhani Wa Ibrahimu (rohoni)..

Waebrania 7:21-25

[21](maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;)

[22]basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

[23]Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae;

[24]bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.

[25]Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Hivyo sisi tuna Neno la ahadi..kwamba tunaomwamini tunapokea uzima wa milele kama yeye.. Lakini pia jambo Hilo amelikolezea Kwa kiapo kuwa hatalibatilisha..Ni hakikisho kubwa sana..Haleluya!

Hivyo ni wajibu wetu kuendelea mbele kwaujasiri na bidiii katika imani na kumtumikia yeye kwasababu yupo pamoja nasi, wala kamwe hawezi kutuacha hata Iweje.

Kwasababu Neno lake ni hakika, alilotuahikikishia Na kiapo juu.

Je umempokea Bwana Yesu kwenye Maisha yako?. Fahamu kuwa hakuna tumaini lolote nje ya Kristo. Okoka leo.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments