Biblia haitoi umri fulani maalumu kwamba mtu akiufikia huo basi ndio huitwa kijana.. Japokuwa ni mtu ambaye yupo umri wa hapo katikati yaani utoto na utu uzima, lakini hutambulika kwa kuangalia vitu kama hatua za ukuaji wake, uwajibikaji wake na uzoefu wake wa kimaisha.
Kwamfano katika biblia watu hawa walitajwa kama vijana.
Na wengine kadha wa kadha..
Yafuatayo ni Mambo ambayo kijana yeyote anatarajiwa awe nayo kibiblia.
Mhubiri 12:1
[1]Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.Â
Zaburi 119:9
[9]Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.Â
1 Timotheo 4:12
[12]Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
Mithali 20:29
[29]Fahari ya vijana ni nguvu zao,..
1 Yohana 2:14
[14]Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Lakini pia kijana anakabiliwa na tamaa za ujanani kama vile uzinzi, anasa,starehe..hivyo Anatarajiwa azikimbie wakati wote.
2 Timotheo 2:22
[22]Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Kutokana na vigezo hivyo tunaweza Kuona ujana pengine huanzia umri wa kubalehe, mpaka wakati mtu anapungua Nguvu zake mwilini.. labda Miaka 12-45…japo yaweza kupungua au kuzidi..
Ikiwa wewe ni kijana, hakikisha maonyo hayo unayatendea kazi mapema…
Lakini ikiwa wewe ni mzazi na una mtoto, fahamu kuwa siku moja atakuwa kijana,hivyo kabla adui hajamtumia, anza kumjengea misingi mizuri ya kutembea katika Imani ya wokovu, naye hataicha njia hiyo mpaka atakapokuwa mtu mzima
Mithali 22:6
[6]Mlee mtoto katika njia impasayo,
Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je Bwana YESU alikuwa na amri ya kumwingiza mtu katika ufalme wa MUNGU au hakuwa nayo?
Fahamu maana ya Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima;Â
About the author