Fahamu maana ya Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; 

Fahamu maana ya Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; 

SWALI: Nini maana ya;

Mithali 10:5 Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima; Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha. 

JIBU: Kwa kawaida kipindi cha hari ( kiangazi), huwa ndio kipindi cha mavuno mengi. kwasababu mavuno yanakuwa yameshakomaa na kukauka.

Hivyo wakulima wengi kwa nyakati hizo wanakuwa mashambani kuvuna, kama vile tu walivyokuwa wakati wa masika walipokuwa wanapanda..

Na ni kipindi ambacho mkulima hufurahi pia kwasababu anakwenda kuona matunda ya kazi yake wakati si mwingi.

Lakini ni ajabu kuona, mtu ambaye hajasumbukia kupanda, halafu anaambiwa tu yeye akavune, tena kwa faida yake mwenyewe akauze, anaona uvivu kwenda kuvuna, hataki kabisa kwenda kujishughulisha na kazi hiyo, mpaka msimu mwingine unakuja, mazao yanaharibikia yote shambani. Mtu kama huyo utamchukuliaje? Ni sawa tu akiitwa  “mwana mwenye kuaibisha”, Kwasasababu ni uvivu wa makusudi.

Sasa jambo kama hili kwasasa lipo pia rohoni.

Na lipo kwa namna mbili.

1.) Katika kazi ya Mungu.

Bwana Yesu alisema..

Yohana 4:35-38

[35]Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. 

[36]Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja. 

[37]Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine. 

[38]Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao. 

Umeona? Kufuatana na vifungu hivyo Bwana anatuonyesha kuwa tupo wakati wa mavuno sasa, wakati wa hari, wa kiangazi, mashamba yamekwisha kuwa meupe,  Hivyo sote kwa pamoja kwa moyo mmoja yatupasa tutoke tuanze kuifanya kazi ya Mungu bila ulegevu kwasababu Yesu alishatupa agizo kuu kuwa tutoke tuenende ulimwenguni kote kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi.

Lakini ukilala na kusema huu si wakati, ndugu ni sawasawa na hilo neno unakuwa mwana mwenye kuaibisha. Kila mmoja wetu ameitwa kuwahubiria wengine habari njema za wokovu wa Yesu Kristo, haijalishi upo ofisini, shuleni, ugenini, jeshini, una wajibu wa kuvuna. Shika mundu yako washuhudie wengine habari njema, kwasababu huu ni wakati  sahihi, na hautadumu milele.Hivyo tumia muda vizuri.

2) Katika kipindi cha maisha ulichopo.

Neno la Mungu linasema..

Mhubiri 12:1

[1]Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,  Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo. 

na pia linasema..

1 Yohana 2:14

[14]Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.

Katika umri wako wa ujana ambao una nguvu ndio wakati wa kwenda shambani kumtumikia Bwana wako. ndio wakati wako wa hari, lakini unapokuwa mlegevu, hujishughulishi na Mungu wako, unachowaza ni anasa, starehe, mihangaiko, unasema nitamtumikia Mungu uzeeni, fahamu kuwa wewe ni sawa na mwana mwenye kuaibisha, kwasababu wakati huo utakuwa umeshapita.

Komboa wakati wako, thamini majira uliyopo, etende kazi ya Bwana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

Maana ya Mithali 25:25 Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu 

Nini maana ya Mithali 16:30 Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka;

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments