Wahivi walikuwa ni watu gani?

Wahivi walikuwa ni watu gani?

Jibu:Wahivi” walikuwa ni moja ya mataifa saba (7) yaliyoondolewa na Israeli katika ile nchi ya ahadi.

Mataifa mengine sita (6) yalikuwa ni Wakanaani, Wahiti, Wayebusi, Waamori, Waperizi na Wagirgashi (soma Yoshua 3:10).

“Wahivi” walionekana kuishi sehemu za vilima vya Lebanoni (kaskazini mwa Israeli mpakani).

Waamuzi 3:3 “aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na WAHIVI WALIOKAA KATIKA KILIMA CHA LEBANONI, TOKA MLIMA WA BAAL-HERMONI MPAKA KUINGIA HAMATHI”

Na sehemu nyingine Wahivi waliyoonekana ni katika nchi ya Mispa karibu na Gibeoni

Yoshua 11:3 “na kwa Mkanaani upande wa mashariki, na upande wa magharibi, na kwa Mwamori, na Mhiti, na Mperizi na Myebusi katika nchi ya vilima, na kwa MHIVI PALE CHINI YA HERMONI KATIKA NCHI YA MISPA”.

Hivyo waliishi sehemu zaidi ya moja katika ile nchi, na ndio wale na ndio wale waliowalaghai wana wa Israeli na kuingia nao agano la kutowaua..kwasababu waliwaambiwa wana wa Israeli kuwa wenyewe ni wenyeji wa mbali kumbe pia walikuwa wanaishi karibu..(Soma Yoshua 9:1-27).

Sababu kuu ya Bwana MUNGU kiyatoa mataifa yale saba (7) kutoka katika nchi ya ahadi ni maovu waliyokuwa wanayatenda..

Walikuwa wanafanya uchawi, mauaji, uasherati, maonezi, dhuluma na mambo mengine mabaya bila hofu yoyote…hiyo ikawa sababu ya kwanza kuwaondoa katika ile nchi…na sababu ya pili ni ahadi Mungu aliyompa Ibrahimu.

Kumbukumbu 9:4” Usiseme moyoni mwako, BWANA, Mungu wako, atakapokwisha kuwasukumia nje mbele yako, ukasema, Ni kwa haki yangu alivyonitia BWANA niimiliki nchi hii; kwani ni kwa ajili ya uovu wa mataifa haya BWANA awafukuza nje mbele yako.

5 SI KWA HAKI YAKO, WALA KWA UNYOFU WA MOYO WAKO, HIVI UINGIAVYO KUIMILIKI NCHI YAO; LAKINI NI KWA UOVU WA MATAIFA HAYA BWANA, MUNGU WAKO, AWAFUKUZA NJE MBELE YAKO; tena apate kuliweka imara hilo neno BWANA alilowaapia baba zako Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.

6 BASI JUA YA KUWA BWANA, MUNGU WAKO, HAKUPI NCHI HII NZURI UIMILIKI KWA AJILI YA HAKI YAKO, KWA MAANA U TAIFA LENYE SHINGO NGUMU”.

Na sababu hizo hizo pia ndizo zilizowatoa Israeli kutoka hiyo nchi ya ahadi na kupelekwa Ashuru na Babeli utumwani.

2 Nyakati 36:14 “Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu.

15 Naye BWANA, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;

16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na kuyadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.

17 KWA HIYO AKALETA JUU YAO MFALME WA WAKALDAYO, ALIYEWAUA VIJANA WAO KWA UPANGA NYUMBANI MWA PATAKATIFU PAO, ASIWAHURUMIE KIJANA WALA MWANAMWALI, MZEE WALA MKONGWE; AKAWATIA WOTE MKONONI MWAKE

Na sababu hizo hizo ndizo zinazotutoa wengi leo kutoka katika ahadi na baraka Mungu alizotuahidia na kujikuta tupo katika laana.

Kumbuka siku zote...SUMU ya kwanza wa Mtu ni DHAMBI na wala si shetani…kilichomwondoa mwanadamu wa kwanza katika nchinya ahadi pale Edeni ni DHAMBI!..

Kilichoshusha maisha ya mwanadamu kutoka umilele mpaka mpaka miaka 120 ni dhambi…hivyo cha kuogopa cha kwanza ni dhambi sio shetani…kwasababu shetani anatumia dhambi kumwaribu mwanadamu.

Hivyo mtu akiweza kuishinda dhambi kwa kudumu katika neno la Mungu, shetani anabaki kuwa kama karatasi tu…hana nguvu yoyote..ni sawa na askari aliyepokonywa silaha.

Kanuni ya kuishinda dhambi ipo kwa Bwana YESU tu na inaanza na TOBA kisha UBATIZO SAHIHI na mwisho UJAZO WA ROHO MTAKATIFU. (Matendo 2:38)

Mtu akiweza kukamilisha hatua hizo tatu kwa kumaanisha kabisa dhambi haiwezi kumshinda na atadumu daima katika ahadi na baraka za Mungu, bila kutumia mafuta,au chumvi au udongo ujulikanao kama wa upako.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Wahiti ni watu gani?

Wayebusi walikuwa ni watu gani?

Edomu ni nchi gani kwasasa?

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments