Hizi ni sababu kuu nne (4), ambazo zinampa sababu mwaminio yoyote kuihubiri injili kwa nia yote kutoka moyoni.
Marko 16:15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”
Bwana wetu alituagiza, na kutupa jukumu la kufanya sisi kama wakristo. Sio tu kusema sisi tumeokoka halafu basi, hapana bali ni pamoja na kuwafanya wengine kuwa kama sisi, kuwafanya kuwa wanafunzi wa Kristo.
Mitume walikuwa na ujasiri wa kumuhubiri Kristo, kwasababu ya ushuhuda wao wenyewe kwa mambo waliyoyaona kwa Bwana Yesu akiwatendea.
Matendo 4:18 Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. 19 Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; 20 maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.
Matendo 4:18 Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu.
19 Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;
20 maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.
Ukisoma pia 1Yohana 1:1-3 Mtume Yohana anasema..
1Yohana 1:1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima; 2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu); 3 HILO TULILOLIONA NA KULISIKIA, TWAWAHUBIRI NA NINYI; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
1Yohana 1:1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
3 HILO TULILOLIONA NA KULISIKIA, TWAWAHUBIRI NA NINYI; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
Hii ikiwa na maana, kuwa kila mkristo aliyekombolewa, anaoushuhuda wa mambo makuu aliyotendewa na Yesu tangu siku alipookoka, Tofauti kubwa aliyoipata katika maisha yake mpya ukilinganisha na yale ya zamani, jinsi mizigo yake ilivyotuliwa, hofu kuondolewa, magonjwa yake kuponywa, kufunguliwa, kupokea furaha ya wokovu isiyo na kiasi, amani, utulivu. N.k.
Yote haya kwa mkristo anayethamini wema wa Mungu hataona aibu kutamani na wengine wauonje uzuri huo ulio katika Kristo Yesu. Na hivyo atatoka nje! na kwenda kuwahubiria wengine Injili ya Yesu Kristo,kama mitume walivyofanya.
Hili lilimkuta mtume Paulo, Hapo mwanzoni alidhani yeye ndio anayekwenda kuwashawishi watu kuhusu Yesu, lakini siku moja aliona maono, watu wa mbali Makedonia wakiwa na uhitaji mkubwa sana wa kumjua Mungu. Hivyo akalitii ono lile akaenda.
Matendo 16:9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. 10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
Matendo 16:9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie.
10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.
Hata sasa, wapo watu wengi wana kiu ya kuijua njia ya kweli, mioyoni mwao wakiwa na shauku ya kuifahamu hiyo NJIA. Lakini sisi tukikaa na kusema hakuna mwenye haja, twajidanganya. Hatupaswi kuona watu kwa nje wanatuchekea, wanafurahi, wana raha, tukadhani hali zao rohoni ndio hivyo zilivyo, tukapuuzia kuwahubiria injili. Wengi wapo kwenye vifungo na wanatamani wapate msaada wa kutoka huko, hawasemi tu. Na anayeweza kuwatoa hapo ni Kristo tu peke yake. Siku ukizungumza nao ndio utajua kweli walikuwa na haja na Kristo. Hivyo usichague wa kumshuhudia. Fahamu tu watu wana haja na kuujua ukweli. Hubiri injili ya Kristo.
Tunajua mtu akifa nje ya Kristo, hakuta tumaini, ni moja kwa moja jehanamu. Tengeneza picha ndugu zako uwapendao, rafiki zako, wazazi wako, na wanadamu wenzako wanakwenda kwenye moto wa milele. Wewe una raha gani leo hii usiwashuhudie habari za Yesu Kristo?.Embu tengeneza picha habari ya Yule tajiri na Lazaro, (Luka 16:19-30) alitamani, mtu atoke kuzimu akawahubirie watu injili ili wasifike mahali pale pa mateso, lakini akaambiwa wapo Musa na manabii huko duniani (ambao ndio sisi), tuwahubirie.
Hivyo kwa sababu hizo kuu nne (4), wewe kama mwaminio uliyeokoka, huna budi kuwashuhudia wengine habari za Kristo. Utasema mimi sina uzoefu, Kumbuka Yesu haitaji uzoefu wako, kuwaokoa watu, kwasababu hata wewe hukuupokea kwa uzoefu wowote, anahitaji kuwaambia Yesu anasemehe dhambi, anaokoa wanadamu, anatoa uzima wa milele bure, anatuepusha na hukumu ya milele, anatua mizigo ya watu, anafariji, anaponya roho, anatupa nguvu ya kuushinda ulimwengu na dhambi. Njoo kwake, akufanye kiumbe kipya upokee uzima wa milele. Hivyo tu. Na hayo mengine mwachie yeye, usifikiri fikiri atakuongoza kwa jinsi utakavyokuwa unasema.
Mathayo 10:20 “ Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”.
Anza sasa.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
NI INJILI GANI UNAHUBIRI?
INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
NJIA KUU YA KUINGIA KATIKA ULE MJI.
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
Rudi nyumbani
Print this post