Edomu ni nchi gani kwasasa?

Edomu ni nchi gani kwasasa?

Swali: Edomu ni wapi kwa sasa?


Maana ya “Edomu” ni “mwekundu”.. Asili ya jina hili kabla halijawa jina la Taifa, ni mwana wa kwanza wa aliyeitwa “Esau”. Biblia inasema Esau alipozaliwa alikuwa mwekundu mwili mzima kama vazi la nywele, tofauti na ndugu yake Yakobo!.

Mwanzo 25:21 “Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.

23 Bwana akamwambia, Mataifa mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.

24 Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake.

25 Wa kwanza akatoka, NAYE ALIKUWA MWEKUNDU MWILI WOTE kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau”.

Baadaye Esau ambaye aliitwa jina lingine “Edomu”(Soma Mwanzo 36:8 na 25:30 na 36:19) alisafiri pande za kusini pamoja na familia yake na Bwana akawabariki na kuzaliana na kuwa Taifa kubwa, na ndipo Taifa hilo likaitwa Edomu, kufuatia jina la baba yao Esau, kama tu vile Taifa la Israeli linavyoitwa leo, kufuatia jina la baba yao Yakobo, aliyeitwa Israeli.

Mwanzo 36: 1 “Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu.

2 Esau alitwaa binti za Kanaani, kuwa wakeze; Ada, binti Eloni, Mhiti, na Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, Mhivi;………………………………

6 Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng’ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; AKAENDA MPAKA NCHI ILIYO MBALI NA YAKOBO NDUGUYE.

7 Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao.

8 Esau AKAKAA KATIKA MLIMA SEIRI, ESAU NDIYE EDOMU.

9 Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri”

Eneo la Edomu kwa sasa ni sehemu katika nchi ya Yordani upande wa kusini magharibi na  katika nchi ya Israeli upande wa kusini, Taifa hili kwasasa halipo tena!!, lilishapotea… isipokuwa eneo Taifa hilo lilipokuwepo ndio sasa linamilikiwa na Israeli pamoja na Yordani katika upande wa kusini wa nchi hizo mbili.

Kufahamu unabii na ujumbe tunaoweza kuupata kupitia Taifa hili la Edomu soma kitabu cha Obadia, au fungua hapa >>>VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 14 (Yoeli, na Obadia).

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

NG’OMBE MWEKUNDU ALIYEZALIWA ISRAELI, ANAFUNUA NINI?

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

SINA PESA SASA, YESU ATANISAIDIA NINI?

MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments