SWALI: Naomba kufahamu Tafsiri vifungu hivi Mhubiri 4:13-16, isemayo ‘Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki’ Nini maana ya habari ile?
Mhubiri 4:13 Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo.
14 Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki; naam, hata katika ufalme wake alizaliwa hali ya umaskini.
15 Nikawaona wote walio hai waendao chini ya jua, ya kwamba walishikamana na huyo kijana, huyo wa pili aliyesimama badala ya yule.
16 Hawakuwa na kikomo hao watu wote, hao wote ambao alikuwa juu yao; lakini hata hivyo wale wafuatao baada yake hawatamfurahia. Hakika hayo pia ni ubatili, na kujilisha upepo.
JIBU:
Mstari wa 13. Unazungumzia jinsi hekima, ilivyo bora kuliko cheo, au umri wa mtu. Yawezekana mtu akawa na vyote, lakini akipungukiwa na hekima, ni hatari kubwa sana, Na dalili moja wapo ya kupungukiwa hekima kama anavyofafanua mhubiri ni kukataa kupokea maonyo.
Mfano wa viongozi wa namna hii kwenye biblia ni Rehoboamu(mtoto wa Sulemani), Nebukadreza (nyakati za mwanzoni), Belshaza, Ahabu, Herode. Unaweza kuona jinsi utawala wao ulivyokuwa mwiba mkubwa kwa taifa, na wengine hata kwa vizazi vya mbeleni, kwasababu hawakukubali maonyo ya ki-Mungu..
Ni lazima tukubali kufundishika, kwasababu huo ndio msingi wa hekima (Mithali 13:1, 13:18, 15:5)
Lakini mstari wa 14
Anaeleza, jambo lingine, linalohusiana na ubatili… anazungumzia habari ya kijana aliyetoka katika umaskini, mpaka kuwa mfalme, aliyetoka vifungoni mpaka kuwa mfalme..
Kufunua kuwa mafanikio ya mwanadamu hayatabiriki, sio tu walio na cheo, au waliozaliwa katika familia ya kifalme, ndio wanaofanikiwa, Bwana anaweza kumwinua maskini, mtu asife faa, na kumfanya mtawala na mkuu, mfano wa Yusufu, na Daudi.
Pia Mstari 15,
Unaeleza kuinuka kwa mtawala mwingine, baada ya huyo kijana. Halafu watu wakashikamana naye huyo..Kuonyesha kuwa sifa za kibinadamu, huwa hauzidumu, maana yake kuwa hata uweje shujaa, ufanye mambo mazuri kiasi gani, utafurahiwa kwa kitambo tu, baadaye utachokwa, siku atakaponyanyuka mwingine, atapendwa, na kufuatawa..na wewe utasahaulika..
Mstari 16
Unaendelea kusema, bado watu waliendelea kumfauta huyo mfalme mpya, yaani walimfurahia pia sawa tu na walivyofurahiwa wafalme wengine nyuma waliopita, lakini ghafla baada ya muda wakamchoka naye pia..Mzunguko ukawa ni huo huo..
Ndipo mhubiri anahitimisha kwa kusema ni ubatili mtupu..Maana yake heshima, sifa, na mapokeo ya kibinadamu hayana umilele nyuma nyake, ni sawa tu na kufuata, upepo, ambapo unaweza kukupa matumaini ya muda, kukupelekea mbali, lakini katikati ya safari, ukayeyukia mbali na usijue unapokupeleka.
Haya ndio mambo tunayoyaona hata sasa katika ulimwengu, ni rahisi sana kuona watu wakimfurahia kiongozi mpya, tena yule mpambanaji, lakini baada ya muda wanaanza kupoteza furaha naye, na hatimaye kumpinga, wakitaka mwingine, na yule mwingine ajapo, huwa vivyo hivyo, wanamfurahia kwa muda, baadaye wanamchoka, mzunguko huo umekuwepo ulimwenguni wakati wote..
Lengo lao ni wakitumainia, kumpata kiongozi bora, lakini hajawahi kutokea..
Hawajui kuwa yupo kiongozi bora, mwema, asiyechokwa, asiye na hila, asitafuta vya kwake, aliyejitoa nafsi yake yeye mwenyewe, anayedumu milele, ambaye huyo mwanadamu akimkubali basi matarajio yake yanafikiwa, kwasababu ankuwa naye wakati wote moyoni mwake.. Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.
Amwaminiye, anapokea uzima wa milele. Wengine wote unafuata upepo..
Je! Upo tayari kumpokea leo, Kama ni ndio, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Maana ya Mhubiri 9:18 Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita;
Nini maana ya hekima ya maskini haisikilizwi? (Mhubiri 9:16)
About the author