Mtume Paulo, alipokamatwa kule Yerusalemu na kupelekwa mbele ya wafalme kuhukumiwa, tunaona ujasiri wake ulikuwa wa ajabu, badala atumie nafasi ile kujitetea, kimahakama, kinyume chake alitumia nafasi ile kuhubiri injili, kiasi cha kumfanya mfalme Agripa kushawishwa kwa muda mfupi kuiamini injili.. Ujasiri wa namna hiyo hakika, ni wa kuigwa sana.
Matendo 26:28
25 Lakini Paulo akasema, Sina wazimu, Ee Festo mtukufu, bali nanena maneno ya kweli na ya akili kamili. 26 Kwa maana mfalme anajua habari za mambo haya, nami naweza kusema naye kwa ujasiri, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni. 27 Mfalme Agripa, je! Wawaamini manabii? Najua ya kuwa wawaamini. 28 AGRIPA AKAMWAMBIA PAULO, KWA MANENO MACHACHE WADHANI KUNIFANYA MIMI KUWA MKRISTO. 29 Paulo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba, ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi, si wewe tu ila na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi, isipokuwa vifungo hivi.
Lakini Tunaona jambo moja, huyu mfalme Agripa alichomwa sana na maneno ya mtume Paulo, alishawishwa ipasavyo na injili ile, lakini hakuwa tayari kugueka moja kwa moja kwa Kristo, aliishia tu kushawishwa.. Ukweli ni kwamba mtu katika hatua hiyo bado hujaokolewa..
Ni sawa na leo hii, watu wengi wanapoisikia injili, ni kweli wanashawishwa, wanaiheshimu, wanaifurahia, wanachomwa mioyo yao, wengine wanaomboleza na kuhuzunika juu ya dhambi zao, lakini je! Wameikubali na kutii?
Utaona wataishia tu kusema, nimebarikiwa!, wataishia kusema Neno zuri linaonya!, wataishia kusema, Mungu nisaidie, nimeguswa leo, ndugu hiyo haimaanishi kuwa umeokoka, huna tofauti na Agripa.
Watu walioshawishwa kwelikweli, waliochomwa mioyo, ni lazima utaona kuna kitu cha ziada watafanya watauliza “Tufanyeje ndugu zetu?”
Matendo 2: 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, TUTENDEJE, NDUGU ZETU? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Matendo 2: 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, TUTENDEJE, NDUGU ZETU?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Umeona?, hawakuishia tu kusema “asante Petro kwa Neno” hawakuishia kusema “ubarikiwe mtumishi” ..“Umetujenga mchungaji”. Walisema, tutendeje ndugu zetu?..Tuchukue hatua gani?
Utaona Wakabatizwa, wote siku ileile, wajazwa Roho, Wakadumu katika fundisho la mitume, kila siku. Ndio hao walioisambaza injili ulimwenguni kote.
Leo ndio tunahitaji kuona Kundi la watu wa namna hii, ambao wanachukua hatua ya kumpokea Yesu kikamilifu na kumfuata kwa mioyo yao yote, kimatendo. Na sio kama akina Agripa, ambaye hakuwa na matunda ya kuitii injili.
Saa ya wokovu ni sasa, usiseme kesho nitaokoka, hakuna wokovu wa kesho, acha kujidanganya, bali ni leo. Aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi usifurahie mafundisho, usifurahie miguso ya ki-mahubiri swali ni je umeokoka? Kristo leo akirudi utaenda naye?
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao.
WOKOVU NI SASA
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ