Warumi 8:37 “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda”
Upo ushindi, lakini pia Upo “Ushindi ulio zaidi ya ushindi”
Unaposhindana na Mtu/Watu na kuwashinda hapo unahesabika kuwa ni “Mshindi”.
Hali kadhalika unaposhindana na mashetani/mapepo na kuyashinda hapo unahesabika kuwa ni “Mshindi”.
Lakini unaposhindana na “MUNGU WA MBINGU NA NCHI” na kumshinda huo ni “Zaidi ya ushindi”
Utauliza kivipi?. Je mtu anaweza kushindana na MUNGU aliyemwumba na kumshinda?..jibu ni ndio!.
Yakobo alishindana na watu na MUNGU na kumshinda..
Mwanzo 32:27 “Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo. 28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
Mwanzo 32:27 “Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda”.
Tafsiri ya jina “Israeli” ni “Mshindi”..
Yakobo alizishindani baraka za MUNGU na kuziteka, alishavuka viwango vya kupambana na watu, sasa yupo viwango vya kupambana na MUNGU na kushinda…huyo huwezi kumwita tena mshindi, ni zaidi ya Mshindi.
Kadhalika walio ndani ya YESU kikwelikweli ni “Zaidi ya Washindi” Ni Israeli kwelikweli…wamevuka viwango vya kupambana na watu, wapo viwango vya kupambana na MUNGU na kuteka baraka zao.
Waefeso 3:20 “Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu”
Waliookoka kweli kweli hawana muda na wachawi, kwasababu hao tayari wamewashinda..
Hawana muda na wanadamu wabaya, kwasababu tayari wameshawashinda katika ulimwengu wa roho, lakini wenyewe wana muda na MUNGU na baraka zake, wanazishindania hizo, na wanaposhinda hawaitwi tena washindi, bali Zaidi ya washindi! Haleluya.
Na kumbuka ushindi huu usio na maelezo upo ndani ya mmoja tu ambaye ni YESU KRISTO, na si kwa mwingine..
1 Wakorintho 15:57 “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo”
Hiyo ndio faida ya kuwa ndani ya YESU…
Wachawi hawawezi kukushinda ukiwa ndani ya YESU, Mapepo hayawezi kukushinda ukiwa ndani ya YESU, Watu wanaoshindana nawe hawawezi kukushinda ukiwa ndani ya YESU.
Dhambi haiwezi kukushinda ukiwa ndani ya YESU, Zaidi sana na (mashetani, watu na viumbe vingine vyote), ambavyo vinafanya vita nawe pasipo wewe kujua haviwezi kukushinda, kwasababu wewe ni mshindi na zaidi ya Mshindi.
Unaingiaje katika huu Ushindi?..Kwanza kwa kumwamini Bwana YESU, na kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kubatizwa kisha kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ