WIMBO ULIOANDALIWA WAKATI WA USIKU.

WIMBO ULIOANDALIWA WAKATI WA USIKU.

Zaburi 42:8

[8]Mchana BWANA ataagiza fadhili zake, na usiku wimbo wake utakuwa nami,.. 

Biblia inataja nyakati mbili, ambazo mwamini anazipitia..nazo ni mchana na usiku.

Mchana ni nyakati za matumaini, nyakato za kuona njia, za kufanikiwa, za amani…hizi ni nyakati ambazo Bwana anasema ataagiza fadhili zake…maana ya fadhili ni kujitoa kwa upendo wa juu sana..Mungu huwafadhili watu wake hata katika nyakati za furaha, na amani.

Lakini pia anasema wakati wa usiku wimbo wake bado utakuwa nasi…usiku ni wakati wa huzuni, wakati wa upweke, wakati wa ukame wa kiroho, wakati wa majaribu, na mapito n.k.

Ni nyakati ambazo huoni chochote…kwasababu usiku sikuzote ni nyakati za ukimya na upofu..

Lakini pia huko Bwana anasema juu ya watu wake kuwa WIMBO WAKE, utakuwa pamoja nao.

Wimbo hufunua nini?

Wimbo humaanisha faraja, kicheko, shangwe, yaani hatawaacha wawe kama walio gizani wanyonge, wapweke, bali kama watu wafurahishwao na nyimbo nzuri sana..

Kama mwana wa Mungu, nyakati za majaribu, Bwana yupo pamoja na wewe, nyakati ambazo huzielewi upo wimbo wake ndani yako.

Wakristo wafikiapo hatua hii huukimbia wimbo wa Bwana na kutazama zaidi changamoto zao, shida zao, magumu yao, na mengineyo kana kwamba Mungu amewaacha, 

Lakini kama ukibakisha fikra zako kwake…utaona bubujiko kubwa sana likitiririka ndani yako, kwa jinsi ile ile ulivyokuwa katika nyakati za nuru..

Kwasababu hii ni ahadi yake. Na kamwe hawezi kudanganya. Unapojifunza kutulia uweponi mwa Mungu, kimaombi, kwa kutafakari, uwapo kwenye hizo nyakati hafifu..ghafla tu utaona furaha, amani, ushindi, kicheko, uwepo wa Bwana vinajaa ndani yako.

Kamwe usiukandamize wimbo huu?

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UYATIE MACHOZI YANGU KATIKA CHUPA YAKO EE! BWANA.

JITIE NGUVU KWA BWANA MUNGU WAKO.

MAISHA YA UVUGUVUGU, YANAMFANYA MUNGU AUMWE.

Print this post

About the author

Lydia Mbalachi editor

Leave a Reply