1 Petro 1:23-25
[23]Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. [24]Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka; [25]Bali Neno la Bwana hudumu hata milele. Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
[23]Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.
[24]Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;
[25]Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.
Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Neno la Mungu linatuonyesha mtu aliyeokoka, anatambulika kuwa amezaliwa mara ya pili kwa mbegu isiyo haribika…lakini wengi hawajui makusudi ya kuzaliwa kwa mbegu hiyo ni nini?
Kabla ya kuona mbegu isiyo haribika, ifahamu kwanza mbegu iharibikayo ni ipi..
Katika habari hiyo tunaonyeshwa mbegu iharibikayo mfano wake ni ile ya mwanadamu .maana yake ni kuwa wewe ulizaliwa kwa mbegu ambayo inaanza katika mtoto, kisha ujana wenye nguvu, lakini baadaye utaishia na kuchakaa, na kuchoka kwa kuishiwa nguvu na hatimaye kufa…ndio hapo anasema mwili wote ni kama nyasi hukauka na kuanguka…kwasababu asili ya mbegu hii si ya kudumu daima.
Vivyo hivyo na mbegu nyingine zote za hapa duniani mfano, za wanyama, samaki, mimea zote ni mbegu ziharibikazo huisha ubora kulingana na wakati.
Lakini ukizaliwa kwa mbegu isiyo haribika maana yake ni kuwa ubora wako haupungui wala hauishi kulingana na wakati ..
Mtu aliyezaliwa kwa mbegu hii ambayo ni Neno la Mungu…huwa hazeeki rohoni, haishiwi nguvu wala hafi kiroho..
Lakini utashangaa mtu anasema kazaliwa mara ya pili, hapo mwanzoni alianza vizuri sana na Bwana, anaomba, anasoma Neno, amesimama, anamtumikia Bwana kwa bidii na uaminifu, lakini baada ya muda anaanza kupoa, hatimaye anaacha hata kuabudu na mwisho anakufa kiroho….miaka miwili nyuma alikuwa ameokoka lakini leo ni mtu mwingine kabisa…hapo ni lazima ujiulize je huyu mtu alizaliwa kwa mbegu ipi?
Kama ni mbegu isiyoharibika mbona wokovu wake unaharibika kulingana na wakati ..kikawaida mwamini kwenye maisha ya kiroho hufanyika upya siku baada ya siku, huama kutoka utukufu mmoja hata mwingine imani moja hata nyingine…lakini wewe unaharibika siku baada ya siku, je wewe ni mbegu gani?
2 Wakorintho 3:18
[18]Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
2 Wakorintho 4:16
[16]Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
Ikiwa unajiona wewe umezaliwa kwa mbegu isiyoharibika, basi onyesha hivyo kwa ubora wako wa kiroho na kiiamani kila siku…ikiwa ni mchungaji onyesha mwendelezo wa kulisimamia kundi la Mungu katika nyakati zote iwe ni ngumu na nyepesi, ikiwa ni mwinjilisti, hupaswi kuacha kuhubiri maisha yako yote, ikiwa ni mhudumu wa kanisani, simama katika nafasi yako kwa ubora wote…usiseme yatosha, usiseme nimechoka,.kwasababu hukuzaliwa kwa mbegu ichokayo, isinyaayo, bali kwa Neno la Mungu lidumulo milele. Ikiwa ni mwombaji, usianze kusema hapo zamani mimi nilikuwa nina uimara kimaombi, kinyume chake onyesha vitendo, hata sasa moto wako ni ule ule tena na zaidi.
Unyesha ubora huo na amani ya Bwana iwe pamoja nawe.
Maran Atha.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Shuhuda za Mungu ni zipi?
Bawa la mbuni hufurahi; Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma?
TIA MIZIZI CHINI, ILI UZAE MATUNDA JUU.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ