Je! Adamu aliwasaliana na Mungu kwa lugha ipi pale bustanini?

Je! Adamu aliwasaliana na Mungu kwa lugha ipi pale bustanini?

JIBU: Biblia haijataja lugha gani ilikuwa inatumika pale Edeni, Lakini ni wazi kuwa kulikuwa na lugha Fulani iliyotumika, kwasababu Mungu ametuumba sisi wanadamu tuwe tunawasiliana kwa njia ya kuzungumza, na hatuwezi kuzungumza bila lugha.   Sasa Mwanadamu wa kwanza Adamu alivyoumbwa ni tofauti na wengine tuliofuata..sisi wengine safari yetu ilianzia katika matumbo ya mama zetu lakini sio Adamu. Adamu Mungu alimwumba mkamilifu, maana ya mkamilifu ni kwamba hajazaliwa wala hajarithi, wala hajafundishwa, yaani ameumbwa tayari ana maarifa kichwani mwake. Tofauti na sisi, tunapozaliwa itatuchukua muda mrefu sana maarifa yaingie kichwani mwetu, mpaka tuweze kuelewa hichi na kile…inachukua miaka mingi….

Ndio maana Mungu alipomtengeneza Adamu alimletea wanyama aangalie atawaitaje..Adamu akawapa majina wote pale pale…hakuhitaji kujifunza kwanza herufi na matamshi..pale pale alianza kuzungumza…Huo ni uwezo wa kipekee sana.   Kwahiyo Adamu aliumbwa na lugha tayari kichwani ambayo kwa kupitia hiyo angeweza kuwasiliana na mkewe, wanawe pamoja na Mungu..(Ingawa Mungu ana uwezo wa kuzungumza na sisi pasipo lugha na tukamwelewa).   Na lugha hiyo Adamu aliyoumbwa nayo ni wazi kuwa iliendelea kutumika kwa vizazi na vizazi mpaka wakati wa Babeli..ambapo lugha nyingi ndipo zilipozaliwa..(Mwanzo 11). Kwahiyo kuitambua lugha yenyewe hasaa ni ipi, ni ngumu inawezekana ni moja ya lugha tunazotumia sasahivi, au ilishamezwa ndani ya lugha nyingine na kupotea kabisa..  

Ubarikiwe.


Mada Nyinginezo:

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.

MTU MWENYE KUSITA-SITA KATIKA MAWAZO MAWILI.

ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

DHAMBI YA MAUTI

BEI YA UFALME WA MBINGUNI:

FUVU LA KICHWA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments