Swali: Katika Isaya 53:13 tunausoma unabii wa Masihi (yaani YESU), Kwamba atakuja kugawiwa sehemu pamoja na wakuu…je! hawa wakuu ni akina nani atakaokuja kugawiwa nao sehemu?…na nini kinagawiwa hapo?
Jibu: Turejee…
Isaya 53:12 “Kwa hiyo nitamgawia sehemu PAMOJA NA WAKUU, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini ALICHUKUA DHAMBI ZA WATU WENGI, Na kuwaombea wakosaji”.
Mstari huo ni kweli unamhusu BWANA YESU (Aliye Masihi) na ni rahisi kutafsirika hivi “kwamba kuna wakuu wanaoishi ambao Bwana YESU naye atakuja kupewa sehemu pamoja nao”.
Tafakari hii sio sahihi, na wala sio maana ya maandiko hayo…kwani hakuna mwanadamu yoyote anayeweza kulinganishwa na YESU wakati huu wa sasa na hata baada ya maisha.
Sasa maana halisi ya mstari huo ni ipi?.
Maana ya mstari huo ni hii… “Mungu atamgawia sehemu Bwana YESU na pia atawagawia sehemu WAKUU”…Maana yake Bwana ana sehemu yake na hao wakuu wana sehemu yao..lakini wote watakuwa na sehemu.
Ndio tukiunganisha maneno hayo mawili tunapata sentensi hiyo “ Mungu atamgawia sehemu pamoja na WAKUU”...
Sasa hiyo sehemu ni ipi na hao wakuu ni akina nani?
“Sehemu” inayozungumziwa hapo ni “Mji wa kimbuinguni, Yerusalemu Mpya” (Soma Ufunuo 22:19).
Na “Wakuu” wanaozungumziwa hapo ni watakatifu watakaoshinda siku ile, hao ndio wanaoitwa “wakuu”. (Wale watu wote walioishi maisha ya kujinyenyekeza kama watoto walipokuwa duniani) sawasawa na Mathayo 18:2-3.
Mathayo 18:2 “Ni nani basi aliye MKUU katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”
Soma pia Luka 7:28 utaliona jambo hilo hilo.
Kwahiyo sehemu ya BWANA YESU ni KITI CHA ENZI CHA DAIMA… na sehemu ya watakatifu watakaoshinda, ambao wataitwa wakuu ni YERUSALEMU MPYA.
Na wanadamu wengine ambao hawatakuwepo katika hilo kundi la ‘wakuu’, basi hawana sehemu yoyote katika mji mtakatifu, bali biblia inasema sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti.
Ufunuo wa Yohana 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, SEHEMU YAO NI KATIKA LILE ZIWA LIWAKALO MOTO NA KIBERITI. HII NDIYO MAUTI YA PILI”.
Tujitahidi tukapate sehemu pamoja na Bwana WETU.
Tujinyenyekeze kama watoto, tukatae udunia na kumwamini YESU, tuache dhambi na tuichukie, tutafute haki na kusimama imara.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
About the author