Hilo ndio jambo la kwanza. Kamwe huwezi kumshinda shetani ikiwa upo nje ya Kristo, Ndicho kilichowakuta wale wana wa Skewa, walipotaka kutoa pepo kwa jina la Yesu. Lakini Yule pepo akawaambia Yesu namjua, na Paulo namfahamu, lakini je ninyi ni akina nani?
Matendo 19:13 Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.
14 Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo.
15 Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? 16 Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa.
Wokovu, ni Kristo ndani yako, na kwa huo nguvu za adui zote huyeyuka mara moja. Mtu aliyempokea Yesu, shetani kamwe hamwezi, kwasababu anamwona Kristo ndani yake.
Unaweza ukawa umeokoka, lakini shetani akapata nguvu za kukusumbua kwa majaribu, kwasababu unashindwa kutumiza baadhi ya wajibu wako kwa mwamini, Yesu alisema..
Mathayo 26:41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Yesu ijapokuwa alikuwa ni mkamilifu hana dhambi, alijaribiwa na adui, wewe ni nani usikutane na hayo? Usipokuwa mwombaji, uvivu ukakumeza, unaona shida kuomba kila siku, kuhudhuria mikesha ujue tayari upo majaribuni. Hata kama utajiona upo sawa, fahamu tu hapo ulipo kuna eneo Fulani adui anakusumbua, utakuja kugundua pindi utakapoanza kuwa mwombaji. Na ndio maana maisha ya wokovu hayatengwi na maombi. Shetani akimwangalia mwombaji anaona moto umemzunguka mkali, hawezi jiamulia tu kufanya analotaka kwake.
Warumi 16:19 Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. 20 Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]
Hapo anasema tuwe wajinga katika mambo mabaya. Ni nafasi kubwa kwa Mungu kumweka shetani chini ya miguu yetu. Kwamfano, unapokuwa hujui kuhusu mitindo mipya ya kidunia, sio mfuatiliaji wa miziki ya kidunia, muvi mpya mpya zilizotoka duniani, yaani kwa ufupi unapitwa na mambo ya kidunia yasiyokuwa na maana kwako, kinyume chake, unakuwa na ujuzi na hekima katika mambo ya rohoni jua hapo umemshinda shetani kwa sehemu kubwa. Hana kitu kwako, kwasababu bidhaa zake, huna mpango nazo, hununui chochote kwake. Kuipenda dunia ni kuwa adui wa Mungu, na rafiki wa shetani.
Kuweka Neno sio, kukariri vifungu vingi vya biblia, hapana, bali ni kufahamu “ukweli” (ufunuo) wa kila Neno unaloliweka moyoni mwako. Pale jangwani, Yesu alipokutana na shetani, alimjaribu kwa Neno hilo hilo,lakini Yesu akamwambia kweli yote ipoje.
Mathayo 4:6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. 7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Ni muhimu ukalifahamu Neno la Mungu katika kweli yake, na hiyo huchangiwa na kufundishwa kwa ufasaha Neno la Mungu na waalimu, kwasababu Roho Mtakatifu atasema na wewe kupitia wao. Lakini pia kumpa Roho Mtakatifu nafasi ya moja kwa moja kukufundisha. Vinginevyo adui atakudanganya sana, hususani kupitia manabii wa uongo, kwasababu hulijui Neno vema.
Kulifahamu Neno, na kuijua kweli, ni jambo muhimu lakini bado shetani anaweza pata mianya ya kukunasa endapo hutaweza kulitii Neno. Penda utakatifu, penda kutendea kazi kile unachofundishwa. Yesu alisema, wapo watu wasikiao tu, lakini wapo wasikiao na kuyatendea kazi. Wote hujaribiwa kwa pepo, mafuriko na mvua za shetani. Sasa Yule aliyejijenga juu ya fundisho tu, na sio kutendea kazi fundisho, ndio huyo anayechukuliwa na mafuriko.
Mathayo 7:26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
Mateso mengine huwapata watu kwasababu ya dhambi. Kuishi maisha matakatifu, humnyima adui mlango wa kukushambulia kwa namna yoyote. Liishi Neno.
Watu wengi hudharau ushuhudiaji. Tunapokuwa na moyo mmoja wa kuitenda kazi ya Mungu, adui hawezi kukaa juu ya anga hili, kutupinga. Tunalisoma wapi hilo? Utakumbuka wakati ule Bwana alipowatuma wanafunzi wake wawili wawili kuhubiri, waliporudi kwa furaha, huku wakimwambia Bwana hata mapepo yanawatii. Yesu akawaambia nalimwona shetani akianguka kutoka juu kama umeme. Kuonyesha kuwa kitendo cha wao kuhubiri adui alikuwa anaporomoka kwa kasi sana.
Mathayo 10:17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.
Hivyo ukizingatia mambo hayo sita (6), Utakuwa sio tu umemdhibiti adui kila Nyanja, bali pia umemteka. Ni wajibu wako mimi na wewe kuboresha mahali ambapo hapako sawa, ili kwa pamoja tukaujenge ufalme wa Mungu na kuziangusha kazi za shetani.
Yakobo 4:7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author