KANISA LILILOTAWANYIKA BADO LINAHUBIRI.

KANISA LILILOTAWANYIKA BADO LINAHUBIRI.

Je unafahamu asili ya kanisa la Kristo? Ni vema wewe kama mwamini ufahamu mapito ya Imani yako.

Mpaka leo hii injili iliyotokea Yerusalemu (Israeli) kunifikia mimi na wewe, fahamu kuwa kuna mapito ambayo waliyapitia , ambayo na sisi tunapaswa tuyafahamu ili tuweze kuifikisha injili hiyo kila mahali,duniani kote na kwa vizazi vyote bila kuwa na deni.

Mwanzoni kabisa kanisa lilikuwa mahali pamoja pale Yerusalemu, Lakini dhiki ilipotokea na kuwa kubwa, mpaka watakatifu kuuliwa hadharani mfano Stefano, iliwagharimu wengi wa wakristo wakimbie Israeli na kwenda mbali kwenye mataifa mageni.

Lakini kuondoka kwao haikuwa mwisho wa safari, kwenda kuanza maisha mapya ya utulivu..hapana kinyume chake kule walipofika ugenini waliendelea kulihubiri lile Neno, kama tu vile walivyokuwa nyumbani.

Matendo ya Mitume 8:1,4

[1]Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume…

[4]Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. 

 Umeona asili ya kanisa la Kristo.. Ni sawa na leo, kuhama-hama kwa watu, pengine kwasababu za kikazi, kivita, kimasomo, kijamii n.k. unajikuta unaenda kijiji jirani, mkoa mwingine, au taifa lingine geni. Jiulize Je! Unalihubiri Neno kama kule nyumbani ulipokuwepo au ndio unabadilika tabia.

Kanisa la kwanza halikupoteza ubora mahali popoteugenini..Kwamfano utaona mtume Petro Aliendelea kuandika nyaraka zake  kwa watakatifu walitoawanyika..mataifa mbalimbali, akijua kuwa injili ya Kristo inaendelea,

1 Petro 1:1

[1]Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia; 

Mazingira hayapaswi kuwa kizuizi cha ushuhudiaji wako, kwasababu kanisa halizuiwi na mazingira..Shuhudia Kristo popote ulipo kwasababu popote walipo watu, Mungu yupo hapo. Usipumbazwe na fikra za kusema mimi nilipo nashindwa kushuhudia afadhali kule nilipotoka, hii kazi mpya niliyoipata siwezi kuwashuhudia watu, ndugu hilo si wazo la Mungu. Fikiri Mungu akupe hekima, na hakika utaona upenyo.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Uinjilisti kama agizo kuu la Bwana.

INJILI YA KRISTO HAITANGAZWI KWA HATI MILIKI.

TUTAFUTE KWA BIDII KUKAA NDANI YA YESU.

 

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply