WEWE NI ZAO LA MAHUSIANO NA USHIRIKA.

WEWE NI ZAO LA MAHUSIANO NA USHIRIKA.

Ulishawahi kujiuliza, kwanini Mungu atumie  namna ya “wingi”, alipomuumba mwanadamu, na sio, “umoja”, kama alivyokuwa anafanya kwenye uumbaji wa vitu vingine?

Mwanzo 1:26-28

26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba

Anasema na “tumfanye” mtu kwa mfano wetu, na si “nimfanye mtu”? Ni kuonyesha hali ya asili ya anaye muumba, kwamba si wa kibinafsi, bali ya kimjumuiko..asili yake ni jumuiya. Ijapokuwa ni Mungu mwenyewe ndio aliyemuumba mwanadamu, lakini wazo lake aliwashirikisha Malaika zake, ambao walikuwepo kabla yetu sisi..Ndio maana ya hiyo “na tumfanye mtu”

Ni kufunua kuwa sisi ni zao la muunganiko, na ushirika, na ndivyo ambavyo tunaweza pia kuzaa, au kufanikiwa katika namna hiyo hiyo.. Ndio maana, hata sisi tukitaka kumleta mwanadamu mwenye asili yetu, sio jambo la mtu binafsi kujitakia pekee yake, ni lazima mwanamume, atakutana na mwanamke, kila mmoja atachangia alichonacho, na mwishowe, anatokea kiumbe kama wao. Hiyo ni kanuni..sisi  kuwepo ni kazi ya “mchango” iliofanywa na watu wawili.

Hata katika maendeleo yetu, na mafanikio yetu. Jambo lolote tukitaka lifanikiwe, ni sharti tukubali michango.. Haiwezekani mtu kusimama mwenyewe mwenyewe kufanikisha kila jambo., Ukuaji wa kiroho, unahitaji kanisa,  ukutanapo na watakatifu wenzako,(wawili, watatu, mia) ndipo unajengwa na kukua, tofauti na kujisukuma mwenyewe mwenyewe, hakuna mafanikio .

Vilevile na katika maendeleo ya mambo mengine yote ya mwilini na rohoni, wanaofanikiwa, ni watu wenye kuruhusu, michango, kusaidiwa, kujihusianisha, kujishusha, kujengwa, kufundishwa, kushauriwa, kuwezeshwa, na wengine..Na hatimaye kufanikiwa..Mafanikio ya moyoni yaani furaha, amani, utulivu, ni mahusiano mazuri na mema uliyonayo na wengine, katika ushirika wa Roho Mtakatifu.

Mwanadamu kamili, huishi kwa mahusiano. Kuanzia sasa usipuuzie mahusiano, Jenga mizizi yako vema, tafuta kwa bidii kuishi kwa amani na watu wote (Waebrania 12:14). Kwasababu wewe ni zao la Mahusiano, tangu mwanzo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply