Nini maana ya Israeli?

Nini maana ya Israeli?

JIBU: Maana yake ni “yeye ashindanaye na Bwana”

Siku ile Yakobo alipotokwa na Mungu, kisha akashindana naye usiku kucha bila kumwacha, ndipo yule mtu akamuuliza jina lako nani, akasema Yakobo, akaambiwa hutaitwa tena hilo jina Yakobo, bali Israeli.

Mwanzo 32:28

[28]Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.

Au kwa namna nyingine tafsiri yake ni

“mtu anayeng’ang’ana na Mungu mpaka kuona matokeo”

Ndio jina ambalo kabila zake zote ziliitwa. Leo hii tunaposema taifa la Israeli, tunamaanisha taifa la washindanaji.

Lakini Israeli kwa agano jipya si hii ya mwilini tu.. bali ile ya rohoni ambayo imeundwa na Yesu Kristo mwenyewe..

Warumi 2:28-29

[28]Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili;

[29]bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.

Maana yake ikiwa umempokea Kristo, wewe tayari ni mwisraeli/myahudi.

Na kama ni mwisraeli, jua asili ya jina lako..kuwa wewe ni mtu wa kung’ng’ana na Mungu…sio mtu mwepesi mwepesi…

Usimrajie Mungu katika vitu virahisi rahisi, huyo ndio sababu kwanini tunakuwa na mifungo na mikesha, kudumu uweponi mwa Bwana wakati mwingi, kumtafuta Bwana, sio kwamba yeye ni mgumu kupatikana hapana, bali kwa asili hataki wana walioitwa kwa jina hilo wawe walegevu,

Wengi hulalamika, mbona sioni uwepo wa Mungu, mbona sioni amani ya kutosha ndani, siono furaha ya wokovu, ukiwauliza vipi juhudi yako rohoni…mmoja atasema ratiba yangu huwa ni maombi ya dk 10 kwa siku, kusoma Neno dk 10.. Sasa mtu kama huyu hawezi kuhudumiwa vema na Mungu ikiwa ameokoka…

Ndugu jitambue wewe ni nani! Ikiwa ni mwisraeli, simama kama mtu shupavu kung’ang’ana na Mungu wako, nje ya hapo, tafuta jina lingine na mungu mwingine mwenye vigezo vyake vya kukuhudumia, lakini kama ni waisraeli wa Kristo, basi ni watu wa kuliitia jina la Bwana bila kukoma (Luka 18)

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NINI MAANA YA UKOMBOZI?

Urujuani ni nini? (Wimbo 3:10)?

PALE MAOMBI YANAPOGEUKA KUWA MAPAMBANO.

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply