Mafanikio ni kitendo cha mtu kufanikisha jambo lolote aliloliadhimia liwe baya au zuri.
Mtu aliyedhamiria kununua shamba na akanunua, mtu huyo kafanikiwa (anayo mafanikio katika eneo hilo).
Vile vile mtu aliyedhamiria kufanya mambo mabaya mfano zinaa au ufisadi na akafanikiwa kufanya hivyo pia ana mafanikio, isipokuwa mafanikio yake hayo mwisho wake ni mbaya (yatamwangamiza).
Mithali 1:32 “Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, NA KUFANIKIWA KWAO WAPUMBAVU KUTAWAANGAMIZA”.
Lakini Baraka ni thawabu pekee itokayo kwa Mungu na kumfikia mtu akiwa hapa duniani, na hakuna baraka yoyofe inayoweza kumfikia mtu mbaya,
Tofauti na mafanikio ambayo hata mtu mwovu anaweza kuyapata, kwani hata shetani ana mafanikio ja utajiri lakini hana baraka yoyote, kinyume chake amelaaniwa.
Lakini baraka za MUNGU, ni kwa watu waliokubaliwa na MUNGU, na matokeo ya baraka za MUNGU pia ni mafanikio.
Na zipo aina kuu mbili za Baraka, ambazo ni baraka za rohoni na za mwilini.
Baraka za rohoni ni zile zinazotajwa katika Waefeso 1:3..
Waefeso 1:3 “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo”
Baraka za rohoni matunda yote ya Roho mtakatifu mtu anayoyapata baada ya kupokea wokovu, ambayo tunayasoma katika Wagalatia 5:22.
Na pia zipo baraka za mwilini, haya ni mafanikio katika afya na vitu vya ulimwengu huu (yaani mali).
Kumbukumbu 28:8 “BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako”.
Watu waliompokea YESU, wanayo ahadi ya baraka zote za rohoni na mwilini, ambazo ndani yake yapo mafanikio ya kiMungu.
Kwahiyo kwa hitimisho tunachotakiwa kukitafuta zaidi ni Baraka za MUNGU, na si mafanikio tu..kwani tukizipata baraka za MUNGU ndani yake pia kuna mafanikio.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ