Na tunaona wakati wa mwisho atapewa uwezo wa kutenda kazi miezi 42, hii ni miaka mitatu na nusu, kati ya ile miaka saba ya mwisho ya lile juma la 70 la Danieli. Hichi kitakuwa kipindi cha DHIKI KUU, sasa hivi PAPA anaonekana kama mtu asiyekuwa na madhara yoyote, anakuja kwa njia ya kujipendekeza ili apate nguvu kiurahisi, kama kitabu cha Danieli kinavyomtabiri, leo hii duniani kote anajulikana kama “MTU WA AMANI”, Ni mtu mwenye wafuasi wengi duniani, na aneyekubalika kuliko mwanasiasi yoyote duniani, dini nyingi zimeanza kuvutiwa naye, hata waislamu sasa wanamwona kama ni mtetezi wao mtu anayejali watu wote, PAPA anasema wote tunamwabudu Mungu mmoja ila kwa njia tofauti tofauti (yaani wakristo, waislamu , wahindu, wabudha tunamwabudu Mungu mmoja), angali biblia inasema YESU ndiye njia pekee ya kumfikia Mungu, na cha ajabu umaarufu wake unaongezeka na watu wanamfurahia ili kutimiza ule unabii kwamba “watu wote ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ndio watakaomsujudia.” Na kumsujudia sio kumpigia magoti bali ni kukubaliana na mifumo yake na imani yake.