Paulo alimwambia Timotheo atumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake, Je! tunaruhusiwa na sisi pia kutumia pombe?

Paulo alimwambia Timotheo atumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake, Je! tunaruhusiwa na sisi pia kutumia pombe?

Tukisoma hilo andiko Biblia inatuambia

1Timotheo5:23″ TOKEA SASA USINYWE MAJI TU LAKINI TUMIA MVINYO KIDOGO,KWA AJILI YA TUMBO LAKO,NA MAGONJWA YAKUPATAYO MARA KWA MARA.  

JIBU: Mtume Paulo alivyosema hivyo hakuwa na maana ya kuhalalisha pombe hapana!! kumbuka divai nyakati za zamani ilikuwa na matumizi mengi, ilikuwa inatumika kama dawa kutibia vidonda,n.k. Kwamfano unamwona yule Msamaria ambaye tunasoma habari zake

Luka 10: 33 “Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,

34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia MAFUTA NA DIVAI; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza”.

Unaona hapo?   Na ilikuwa pia ina matumizi mengine mengi, sasa zamani za kanisa la kwanza wakristo wengi walikuwa wanafunga muda mrefu, na kusafiri umbali mrefu kwenda kuhubiri injili, kwasababu kulikuwa hakuna magari wakati ule, au ndege kama tulizonazo sasa , kwahiyo kutokana na hari za jua na majangwa, na kufunga juu yake, wakati mwingine utumbo unakuwa unajisokota, au kunakuwa na udhaifu fulani katika mwili,   Sasa Mtume Paulo kwa kulijua hilo kutokana na uzoefu wa muda mrefu aliokuwa nao wa kusafiri masafa marefu kuhubiri injili, alimshauri Timotheo asitumie maji tu bali na mvinyo(divai) kidogo kwa ajili ya tumbo, na sio kwaajili ya kujifurahisha au kujiburudisha wanavyofanya watu sasahivi,

kwahiyo unaona hapo? anamshauri atumie kama DAWA, ni sio kama kiburudisho, ni sawa na mimi nikushauri wewe unaposafiri mahali palipo na ukame kidogo wa chakula kwa ajili ya injili usinywe maji matupu peke yake, bali unywe kinywaji chenye nguvu kidogo (mfano Energy drink),ili mwili usipungukiwe nguvu njiani. unaona hapo nia yangu sio kukwambia unywe energy drink kila wakati, kujiburudisha hapana bali nia yangu ni kukuzuilia mwili usidhoofike njiani kwa muda ule utakapokuwepo safarini, kutokana na uzoefu nilio nao kusafiri mda mrefu.  

Hivyo mtu yoyote anayeshikilia hilo andiko kiuhalalisha atajua kabisa pombe ni makosa, kwasababu hakuna mtu yoyote anayekunywa pombe kama dawa katika mwili wake,.wote wanakunywa kwa ajili ya tamaa za mwili na ulevi, ambayo ni dhambi na hata hivyo ukiangalia kwa makini utaona pombe zote tulizonazo sasahivi hazina matumizi mengine zaidi ya ULEVI tu, basi zimetengenezwa mahususi kwa ajili ya kazi hiyo na si vinginevyo…Hivyo mkristo yoyote anayekunywa pombe anafanya makosa mbele za Mungu kwa kisingizio cha huo mstari.  

Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

MATUMIZI YA DIVAI.

JE! MABALASI BWANA YESU ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA TU KWA KAZI HIYO?

JE NI SAWA KWA MKRISTO KUUZA MAZAO YA KUTENGENEZEA POMBE KAMA VILE MTAMA?

RABONI!

KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ibrahim pafredi
Ibrahim pafredi
8 months ago

Mafundisho mazuri sana