Je! ni vema kwa mkristo kwenda hospitali au kutumia miti shamba anapougua?

Je! ni vema kwa mkristo kwenda hospitali au kutumia miti shamba anapougua?

JIBU: Kama tukisoma Marko 2: 17 tunaweza kuona Bwana Yesu aliwaambia watoza ushuru na Mafarisayo maneno haya, “…WENYE AFYA HAWAHITAJI TABIBU, BALI WALIO HAWAWEZI; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.” Bwana alitumia mfano huo wa kidunia kueleza mambo ya rohoni, akimaanisha kuwa ni jambo la kawaida kwa mtu aliye mgonjwa kumtafuta daktari amuhudumie afya yake. Kwasasa tunaweza kusema kwenda hospitali. Hivyo mkristo kuumwa na kwenda hospitali hafanyi kosa lolote, maadamu anafanya tendo ambalo halimwathiri Imani yake.  

Kadhalika pia anaweza kutumia aina zozote za mimea ambazo anaweza kuona zitamsaidia kuimarisha afya ya mwili wake, mwingine anaona kutumia mwarobaini, au alovera ni nafuu zaidi kwake kuliko dawa za hospitalini kwasababu pia dawa nyingi za hospitalini zinatengenezwa kutoka kwenye hiyohiyo mimea ya asili. Lakini la kuzingatia mkristo anapotumia dawa hizo, hapaswi kuzihusisha na ibada zozote za Kiroho isipokuwa kwa Mungu wake.  

Kwamfano mtu anapewa dawa za miti shamba labda mwarobaini, halafu anaambiwa achinje kuku, au aweke uvunguni, au aseme maneno Fulani au afanye kafara kisha ndio anywe, sasa hizo tayari ni ibada za sanamu ambazo ni machukizo makubwa mbele za Mungu. Lakini mtu akiwa na mwarobaini wake nyumbani, akatengeneza akanywa kwa jina la YESU hakuna tatizo lolote. Akizingatia tu lile Neno katika

Wakolosai 3: 17 “Na kila mfanyalo, KWA NENO au KWA TENDO, fanyeni yote KATIKA JINA LA BWANA YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.

Lakini pia kuna mwingine kwa Imani yake anaamini kuwa Mungu ndiye mponyaji wake kwa asilimia zote pasipo kupitia nyenzo yeyote, hivyo anaposikia kuumwa anaamini kuwa Mungu atamponya pasipo kwenda hospitali, akiliamini lile Neno (Mathayo 8:17 “…Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.” )

hivyo mtu wa namna hii pia hafanyi kosa, Kwasababu Mungu ni yule yule anayeweza kumponya mtu kwa kupitia daktari au pasipo daktari..Hapo ni kulingana na Imani ya mtu kwa Mungu wake.  

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

YESU MPONYAJI.

HADITHI ZA KIZEE.

MADARAKA YA WAKATI MKAMILIFU.

MKUU WA GIZA.

NGUVU ZA ZAMANI ZIJAZO:

PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
HERY T. NJELEKELA
HERY T. NJELEKELA
2 years ago

Mafundisho mazuri,je nifanye nini ili mungu ajibu maombi yangu.