Je ni sahihi kulima mazao, ambayo hutumiwa kutengenezea pombe?

Je ni sahihi kulima mazao, ambayo hutumiwa kutengenezea pombe?

SWALI: Kwamfano tunajua kuna pombe zinazotengenezwa na mtama Je! ni sawa kwa mkristo wa kweli kulima mtama na kuuza na hata hiyo hela kuitumia kutolea sadaka?


JIBU: Hakuna zao lolote lililoumbwa na Mungu lenye ubaya wowote ndani yake, zao linafanyika kuwa baya pale tu linapotumiwa kwa matumizi yasiyo sahihi, kwamfano mtama ni zao la chakula, wengine wanatumia kama ugali, lakini baadhi ya watu wanatumia fursa ya zao hilo ili kuunda pombe. Hivyo mtu anayeligeuza zao kuwa hivyo , au kupanda kwa ajili hiyo, atakuwa na hatia mbele za Mungu.

Lakini zao lenyewe kama zao halina shida kama mtu akilipanda kwa ajili ya matumizi ya asili, kwasababu yapo mazao mengine mengi tu kwamfano zao kama miwa, ambayo ingetumiwa kutengenezea sukari wengine wanaundia pombe, minazi ambayo ingetumika kuzalisha nazi na mafuta wengine wanaigema kutolea pombe, ulezi na ndizi ambazo zingetumika kama chakula wengine wanatumia kutengeneza pombe n.k. Lakini biblia ilishasema katika, 

Isaya 5:20 Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza; WATIAO UCHUNGU BADALA YA UTAMU, NA UTAMU BADALA YA UCHUNGU!.

Unaona hapo? Biblia imetoa onyo kali kwa wale wote wanaopenda kupundia, vitu ambavyo Mungu aliviumba vitumike ipasavyo katika uhalisia wake, Kuzalisha mtama kwa ajili ya kutengenezea pombe ni sawa na kutia uchungu katikati ya jamii badala ya utamu. Kuzalisha ulezi na ndizi kwa dhumuni la kuviuzia viwanda vya utengenezaji pombe, ni sawa na kutia uchungu katikati ya jamii badala ya utamu. Kadhalika na mambo mengine yote ambayo yangepaswa yatumike kwa matumizi ya asili lakini watu wanayageuza, kwamfano wanaume kwa wanaume, na wanawake kwa wanawake ni sawa na kutia nuru badala ya giza..Bwana alishasema OLE WAO wafanyao hivyo. 

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

JE! TUNARUHUSIWA KUNYWA MVINYO KIDOGO KWA AJILI YA TUMBO KAMA PAULO ALIVYOMWAMBIA TIMOTHEO?

MATUMIZI YA DIVAI.

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.

JE! MABALASI BWANA YESU ALIYOYATUMIA KUGEUZIA MAJI KUWA DIVAI, YALITUMIKA KWA KAZI HIYO TU?

JE! MTU ANAPOFUNGA KWA MUDA WA SAA 24,ANAPASWA KUNYWA MAJI AU KITU CHOCHOTE?


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments