Mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake hawezi kuwa mwanafunzi wangu?

Mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake hawezi kuwa mwanafunzi wangu?

SWALI: Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini katika hivi vifungu?

Luka14:26 “kama mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake,na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; na naam, na hata nafsi yake mwenyewe , hawezi kuwa mwanafunzi wangu ”.


JIBU: Bwana Yesu aliposema yeye “asiyemchukia” baba yake na mama yake, hakumaanisha, kumdharau, au kuweka uadui naye, hapana kwasababu Bwana Yesu hawezi kufundisha upande mmoja upendo na mwingine chuki, bali pale alimanisha kupenda mapenzi ya wazazi au ya mtu binafsi Zaidi ya mapenzi ya Mungu, mtu wa namna hiyo hawezi kuwa mwanafunzi wake.

Leo hii mtu atafahamu kabisa kuwa mlevi au kufanya matambiko ya kimila ni dhambi sawa sawa na Neno lake katika

Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.
13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.

lakini kwasababu mzazi wake anamshurutisha afanye vile kwasababu wazee wa ukoo wameagiza ,na asipofanywa hivyo atatengwa na ukoo, yeye anaamua awe mlevi, au apige ramli ili tu kuwaridhisha wazazi wake. Mtu wa namna hiyo biblia inasema hawezi kuwa mwanafunzi wa YESU.

Kadhalika Bwana anasema mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuuona ufalme wa mbinguni, lakini mtu kwasababu dini ya wazazi wake haiamini hivyo, anaona vema abaki hivyo hivyo tu, angali akijua kabisa ubatizo sahihi ule wa kuzamishwa katika maji tele tena katika Jina la YESU KRISTO ndio Bwana anaouhitaji kwa mtu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zake, lakini yeye hataki kutii akiwaogopa wazazi au ndugu zake..Sasa mtu kama huyu hawezi kuwa mwanafunzi wa YESU.

Na maagizo mengine yote Bwana aliyotupa, hatupaswi tutazame kwanza wanadamu wanatoa maoni gani kuhusu hayo.Kama ni Bwana kasema moja kwa moja tunatii pasipo kuwatazama wanadamu wanasema nini.

Ili kufanyika wanafunzi kweli kweli wa Kristo hatuna budi kuingia gharama, Hivyo Bwana atupe rehema tuweze kuzishinda hatua zote.

Amen.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP

Mada zinazoendana:

JE! NI KWELI UMEMFUATA YESU?

JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.

UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.

UBATILI.

WANA WA MAJOKA.

RACA


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply