Apandacho mtu ndicho atakachovuna

Apandacho mtu ndicho atakachovuna

Wagalatia 6:7 “Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.

8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele”.

Hapo inasema “chochote” ikiwa na maana kuwa hata vitu visivyokuwa na maana vikipandwa vinaleta majibu.

Na chochote kinachopandwa huwa kinapandwa kama mbegu…na kinapovunwa kinavunwa kama tunda…embe linapandwa kama mbegu, lakini linavunwa kama tunda..

Mtu akipanda mbegu ya dhambi yoyote moyoni mwake leo, akaipalilia hiyo tabia moyoni mwake, baada ya muda fulani, atavuna matunda ya dhambi hiyo..Na matunda yake ni ya aina mbili…MAUTI YA MWILI, na MAUTI YA ROHO…

Mauti ya Mwili, inaweza kuja kutokana aidha  Ugonjwa unaotokana dhambi hiyo au janga fulani kwamfano dhambi ya uasherati mauti yake ya kimwili inaweza kutokana na ugonjwa fulani kama HIV, GONOREA au kaswende au inaweza kuja kupitia chanel nyingine yeyote tofauti na hiyo..Wengi hawajui kuwa vifo vingi vya ghafla vinatokana na matokeo ya dhambi…hususani dhambi ya uasherati…

Aina ya pili ya tunda la dhambi ni Mauti ya kiroho. Hii ni ile hali mtu anakufa katika kuisikia Injili na kuiamini, upo usemi unaosema “sikio la kufa halisikii dawa” kadhalika, roho iliyokufa haiwezi kuisikia Injili tena, na mwisho wake ni ziwa la moto.

Jiepushe na uasherati kwasababu apandacho mtu ndicho atakachovuna, jiepushe na ushirikina, ulevi, anasa, ushoga, ulawiti, usagaji, utazamaji wa picha na video chafu, ulaji rushwa n.k kwasababu mambo hayo yote matunda yake ni kifo.

Kwasababu biblia inasema Mshahara wa dhambi ni Mauti.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

JE! KUNENA KWA LUGHA MPYA KUKOJE?

JE! KUOMBA KWA BIDII KAMA ELIYA NI KUOMBA KWA NAMNA GANI?

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOKUJA JUU YA MTU.

USITAFUTE FAIDA YAKO MWENYEWE BALI YA WENGINE.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments