Biblia inasema Nuhu alikuwa na watoto watatu tu! SHEMU, HAMU na YAFETI, ambao wote walikuwa wakiume.
Mwanzo 5:32 “Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi”
Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika”.
Na Hao ndio walioingia kwenye safina pamoja na wake zao.
Mwanzo 7:7 “Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika”.
Hivyo ndani ya safina kulikuwa na watu 8 tu!
Inasikitisha kiasi gani? watu 8 tu ndio waliopona kati ya mabilioni waliokuwa wanaishi duniani?..Mlango wa safina ulipofungwa watu walitamani kuingia lakini wakashindwa.
Na sisi je tutapataje kupona tusipouthamini wokovu mkuu namna hii? (Waebrania 2:3). Na dunia hii ya mwisho biblia inasema watakaopona ni wachache sana, watakaonyakuliwa ni wachache sana..Ni wale tu watakaojitahidi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba
Luka 13.24 “Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
25 Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;
26 ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu.
27 Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu”.
Tujitahidi tuwe mimi na wewe
Maran atha!
Mada Nyinginezo:
NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?
NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?
About the author