NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?

NUHU ALIJENGA SAFINA KWA MIAKA MINGAPI?

Biblia haijaweka bayana safina ilijengwa kwa muda gani, Wapo wanaosema ilijengwa kwa muda wa miaka 120 kufuatia mstari wa kitabu cha Mwanzo 6:3 ” Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.”

Lakini bado hiyo haileti maana kamili..Lakini pia biblia inasema Nuhu aliwazaa watoto wake akiwa na miaka 500,(Mwanzo 5:32) Na inasema aliingia katika safina akiwa na miaka 600, hivyo kufanya tofauti ya miaka 100 hapo, ambayo ndani ya hiyo pengine ndiyo aliyotumia kuijenga safina, lakini pia hoja hiyo ina mapungufu kidogo.

Kwa ufupi ni kwamba biblia haijaeleza ilijengwa kwa muda gani, hivyo pengine ni jambo ambalo halina umuhimu sana kwetu kulijua.

Jambo la Muhimu kujua ni kwamba, Kama dunia ya kwanza iligharikishwa na maji kwa ajili ya maovu ya watu, basi na dunia hii ya pili tunayoishi mimi na wewe nayo pia itagharikishwa vile vile kutokana na maovu ya wanadamu.. Na Biblia inasema haitagharikishwa kwa maji tena bali kwa moto.

Biblia inasema hivyo katika 

2Petro 3:6 ” kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.

7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.”

Dhambi kama uzinzi, rushwa, chuki, fitina, kutokusamehe, ulevi, ushoga, ulawiti, usagaji, utukanaji, tamaa mbaya, utoaji mimba, wizi na nyingine zote ndio iliyoizamisha dunia ya kwanza kwenye maji. Na ndizo zitakazoizamisha dunia hii tunayoishi sasa katika moto. Kama Mungu alipozungumza alitenda kwa Nuhu, kadhalika alivyozungumza sasa katika Neno lake atatenda.

Je! na wewe bado upo ulimwenguni? bado hujampa Kristo maisha yako, na kuacha dhambi? Unyakuo upo karibu sana kutokea.

Bwana akubariki

Ikiwa utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya kila siku, kwa njia ya email, au whatsapp, basi tutumie ujumbe kwenye namba hii : +255789001312


Mada Nyinginezo:

NUHU ALIKUWA NA WATOTO WANGAPI?

NUHU ALIISHI MIAKA MINGAPI?

NUHU ALIWALETAJE LETAJE WANYAMA KWENYE SAFINA?

NUHU WA SASA NI YUPI?.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Nestory J. Kimila
Nestory J. Kimila
2 years ago

Hii nimeipenda. Napenda mafundisho.
Kama nitakuwa nayapata, nitaendelea zaidi kukua kiroho