KWANINI MUNGU ALITUUMBA WANADAMU.

KWANINI MUNGU ALITUUMBA WANADAMU.

Tofauti na sisi wanadamu tulivyo, tukiunda kitu au tukiumba kitu Fulani ni kwa lengo moja tu ni ili kutusaidie sisi kufanya jambo fulani au kitunufaishe kwa namna moja au nyingine. Kwamfano mtu anaunda gari ni ili limsafirishe, anaunda meli ni ili imsaidie kutembea juu ya maji n.k. lakini kwa Mungu haiko hivyo yeye alituumba sisi kwa mapenzi yake/raha yake/furaha yake tu basi, (his pleasure).

Hakupungukiwa na kitu Fulani  na hivyo akatuumba sisi ili kwa kupitia sisi akipate hapana, wengine wanasema Mungu alituumba ili tumwabudu, kusema hivyo sio sahihi , ukweli ni kwamba tunamwabudu Mungu kwasababu alituumba, lakini sio alituumba ili tumwabudu, Mungu hajaishiwa sifa biblia inasema vyote vinatoka kwake..(Zaburi 139)

Wakolosai 1:16 “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake”.

Hivyo fahamu tu kuwepo kwako wewe duniani ni furaha yake, anafurahi kukuona wewe upo kama ulivyo, anafurahia kukuona unafanya mambo mazuri kama yeye anayoyafanya, anafurahia kukuona wewe unayo amani kama yeye aliyonayo, unayo furaha, unao upendo kama yeye alionao, ..hakukuumba ili akutese, au akutumikishe hapana..Lakini ni kwasababu amekupenda tu na ametaka wewe uwepo…

Ni kwa vile tu tulizama katika dhambi, tukajiharibia maisha  wenyewe lakini mapenzi ya Mungu halisi yalikuwa ni milele tuishi ndani ya PENDO lake, lakini pamoja na hayo Pendo hilo limerejeshwa na YESU KRISTO, Kwa kupitia yeye huyo ndio tunaona ni jinsi gani alivyokuwa amtupenda tokea mwanzo….Jaribu kufikiria jinsi alivyomtuma mwanawe wa pekee, kutuokoa sisi tuliokuwa tumepotea, alichukua dhambi zetu, alichukua magonjwa yetu, alichukua masumbuko yetu…

Hata na wewe ukikaa ndani yake basi Pendo hilo nalo litakuja ndani yako..Nawe utamfarahia Mungu wako kama vile yeye anavyokufarahia, utampa sifa wa jinsi alivyokuumbwa kwa utashi wa hali ya juu namna hiyo, utamwabudu kwa uumbaji wake wote ulivyo mkuu, utamtukuza kwa jinsi anavyokulisha na kukupa riziki zako za kila siku..

Zaburi ZABURI 150

1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;

4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;

5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana.

Haleluya.

Pia kwa Maombezi, Ushauri, Maswali au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

YESU NI NANI?

BASI MUNGU AKAMUADHIMISHA SANA.

JE! KUBET NI DHAMBI?

NI KWANINI MUNGU HAONEKANI?

UNYAKUO.

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
mabel
mabel
3 years ago

HABARI, Kama ametuumba tu kwa ladhi yake au furaha yake na si kumwabudu kwanini anatuambia tusiabudu miungu wengine?