Katika Biblia Injili ni nini maana yake?
Neno Injili limetokana na Neno la kigiriki “euaggelion” lenye maana ya “Habari Njema”. Hivyo Injili maana yake ni habari njema…Tukirudi katika biblia Injili maana yake ni “Habari Njema za Yesu Kristo”
Luka 2:8 “Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku.
9 Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang’aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu.
10 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;
11 maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana“.
Habari yoyote inayomhusu Bwana Yesu Kristo, kuzaliwa kwake, kuishi kwake, mahubiri yake, kufa kwake na kupaa kwake, na kurudi kwake mara ya pili hiyo ndiyo Injili ya kweli na ndio habari njema.
Injili ya kweli ina nguvu ambayo inaleta wokovu..
Warumi 1:16 “Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.
Kinyume chake injili yoyote isiyomwelezea Yesu kuzaliwa kwake, kuishi kwake, kufa kwake, kupaa kwake na kurudi kwake mara ya pili, injili hiyo ni injili ya uongo ya yule Adui shetani ambayo katika nyakati hizi za mwisho imezagaa kila mahali.
Injili ya uongo inaelekeza kutafuta na kuyapenda mambo ya ulimwengu huu, haielekezi Toba na msamaha wa dhambi, Injili ya uongo haizungumzii hata kidogo kurudi kwa Kristo mara ya pili, badala yake inawalewesha watu wasikumbuke wala kufahamu kuwa Yesu Kristo atarudi tena kama alivyosema..
Injili ya uongo kamwe haigusii kwamba tunaishi katika siku za hatari na za mwisho, siku zote inafundisha kuwa bado sana mpaka mwisho ufike. Na injili hii inahubiriwa na wanadamu, ipo injili nyingine inayohubiriwa na vitu vya asili ijulikanayo kama Injili ya Milele, ambayo hatuna nafasi leo ya kuizungumzia hapa…
Injili (au Habari Njema) sasa imeshahubiriwa katika mataifa yote, hakuna nchi ambayo Injili ya kweli ya Yesu Kristo haijafika, hivyo ule mwisho umekaribia sana, tunaishi katika muda wa nyongeza, saa yoyote wakati wowote Unyakuo utapita. Je una uhakika wa kunyakuliwa endapo parapanda ikilia leo? Jibu unalo
Mathayo 24:14 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
USIPOLITENDEA KAZI NENO LA MUNGU.
About the author