Je! Adamu alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Lilith?

Je! Adamu alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Lilith?

Je! Adamu alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Lilith?


JIBU: Biblia imetupa majibu kama ifuatavyo..

Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMUME NA MWANAMKE ALIWAUMBA.  

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.

Huo ni mstari wa kwanza kabisa unaozungumzia uumbaji wa mwanadamu katika biblia, hakuna mstari mwingine kabla ya huu.. Na unasema Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. (maneno hayo mawili yapo katika umoja.). Na haijasema Mungu alimwumba Mwanaume na wanawake.. wala haijasema Mungu alimuumba mwanamke na wanaume. 

Kwahiyo hakukuwa na mwanaume Zaidi ya Adamu, na wala hakukuwa na mwanamke mwingine Zaidi ya Hawa katika uumbaji.

Jambo linalowachanganya wengi ambalo ndilo limezua swali hili, ni kuhusu mke wa Kaini, kwamba Kaini alitolea wapi mke?

Kwanza kabisa Ni muhimu kufahamu kuwa Adamu na Hawa, walizaa Watoto wengine wengi wakike na wa kiume baada ya Habili na Kaini. Watoto wa Adamu hawakuwa wawili tu, bali wengi.

Mwanzo 5:4 “Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa”.

Kwahiyo miongoni mwa hao Watoto wa kike aliowazaa Adamu, mmojawao ndio alikuwa mke wa Kaini, na Kaini na mkewe walizaa Watoto, na watoto wao walizaa Watoto, na wajukuu zao pia walizaa..Na wakati huo watu walikuwa na uwezo wa kuishi mamia ya miaka.

Kwahiyo ni uongo kusema kuwa Adamu alikuwa na mke mwingine tofauti na Hawa.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

BUSTANI YA NEEMA.

 

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Jeremy
Jeremy
1 year ago

BINADAMU WA KWANZA
Mwanzo 1:27 mungu akaumba mtu kwa mfano wake (aliwaumba mwanamume na mwanamke)
BINADAMU WA PILI?
Mwanzo 2:7 mwanaume alifanywa kwa mavumbi ya udongo na mungu akampulizia puani pumzi ya uhai. 2:21-22 ni pale mwanamume anakuwa katika uzingizi na mungu anachukua ubavu wake na kumuumba mwanamke. KUMBUKA BINADAMU WA KWANZA WOTE WALIUMBWA ZIKU MOJA; BINADAMU WA PILI MWANAMUME ANAUMBWA WA KWANZA NA BAADA YA KUWA MPWEKE MUNGU AKAUMBA MWANAMKE…Tafathali naomba maelezo zaidi nipate kuelewa

Samuel
Samuel
4 years ago

MOHAMED UNALETA SHAURI KWA SAMSON AU LA! NI SWALI KAMA SWALI ZINGINE?

Mohamed kassim
Mohamed kassim
4 years ago

Shalom me ninavyojua hakukuwa na uzao wa Adam peke yake.
Ule ulikuwa uzao wa MUNGU alafu kuna uzao mwingine ulikuwepo.
Ndio maana BWANA MUNGU hakumwambia Adam akazae ili aongezeke. Ila yupo mwingine Aliyemuumba Akamwambia akazae aongezeke Mwanzo 1:26.

Sasa Kama ni hivyo kwa nini MUNGU Awalaani kwa kula tunda???
Na ukweli wa hilo tunda lilikuwa ni uzinzi ingawa imefichwa. Ila huo ndio ukweli ukitaka kuelewa kwanza angalia hoja zangu:

01: MUNGU alilaani Kati ya uzao wa Hawa na nyoka akaweka uadui Kati ya mizao yao. Mwanzo 3:15.

02: MUNGU Alimwadhibu mwanamke katika uzazi wake kwa nini owe hapo tu na sio kwa namna nyingine????
Pia me sijaona sehemu ambayo MUNGU alimwambia Adam akazae na kuongezeka sijaona.

03: Jambo lingine ni kujigundua kuwa wapo uchi. Hili limenifanya nifikirie Sana kitu gani kilichopelekea kujua kuwa wapo uchi???

Samson makungisa
Samson makungisa
4 years ago

Je! Ilikuwa ilitoka kwa mungu kuwa kaini ajitwalie binti kati ya babaye na azaye naye na ule binti akubali tumbo yake izae laana Kupitia kaini?