Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu.
Warumi 6:8 “Lakini tukiwa TULIKUFA PAMOJA NA KRISTO, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye”
Kabla ya kujitathmini kama kweli tulikufa pamoja na Kristo hebu kwanza tukitafakari kifo cha Bwana Yesu.
Tunasoma kifo cha Mwokozi wetu hakikuwa cha ugonjwa, au cha uzee, au cha ajali… bali kilikuwa ni kifo cha mateso, Bwana Yesu alibeba msalaba wake mpaka Golgotha, na pale akatundikwa msalabani kwa dhihaka nyingi na maumivu makali na kwa masaa mengi.
Lakini pamoja na hayo alisema kuwa “mtu yeyote akitaka kumfuata, ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake ndipo amfuate..
Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate”.
Nataka tutafakari kwa undani mambo hayo matatu (3), kujikana, kubeba msalaba na kumfuata Yesu…
1. Ajikane mwenyewe.
Maana ya kujikana, ni kukataa mapenzi yako na kujiachilia kwa mapenzi ya mwingine, hivyo Kristo anataka mtu yeyote anayetaka kumfuata ni lazima ayaache yale anayoyapenda na kuyafuata yale yeye (Kristo) anayoyapenda.
2. Ajitwike Msalaba wake.
Kujitwika msalaba maana yake ni kubeba kitu ambacho utakwenda Kuteswa nacho. Kristo alibeba msalaba wake na akaenda kusulubiwa juu ya huo, na ndivyo sisi nasi tunapaswa tubebe misalaba yetu..
3. Anifuate
Amfuate wapi?…amfuate kila mahali atakapokwenda… na mwisho wa safari ya Yesu ni Golgotha, katika Kifo!….na kifo cha Bwana Yesu kilikuwa juu ya ule msalaba alioubeba, na si juu ya kitu kingine chochote, vile vile na sisi tunaposema tumekufa pamoja na Kristo ni lazima kifo chetu kiwe juu ya misalaba yetu tuliyoibeba na si juu ya kitu kingine chochote.
Je umeubeba msalaba wako?
Kama hukuubeba msalaba wako utasemaje basi ulikufa pamoja Kristo?.. Kama hujajikana nafsi utasemaje kuwa umekufa pamoja na Kristo?, Kama mapenzi ya baba yako yana nguvu kuliko mapenzi ya Mungu utasemaje ulikufa pamoja na Kristo?.. Kama unamwogopa mama yako kuliko kumwogopa Mungu utasemaje ulikufa pamoja na Kristo?… Kama kazi yako ina nguvu kuliko ibada za Kristo utasemaje ulikufa pamoja na Kristo?, kama kumkiri Kristo tu mbele ya watu ni ngumu utasemaje ulikufa pamoja naye?, kama maisha yako yamejaa uchafu wa kila aina utasemaje basi ulikkufa pamoja na Kristo?.. Wengi wamekufa pamoja na Yuda katika roho lakini si pamoja na Kristo, waliokufa pamoja na Kristo ni watu waliobeba misalaba yao..
Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 MTU YE YOTE ASIYEUCHUKUA MSALABA WAKE NA KUJA NYUMA YANGU, HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU”.
Na wote waliokufa pamoja na Kristo na kuzikwa pamoja naye ndio watakaoishi pamoja naye kama maandiko yanavyosema…
Warumi 6:8 “Lakini tukiwa TULIKUFA PAMOJA NA KRISTO, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye”
Je wewe umekufa pamoja na nani?.. na umekufa juu ya nini?….Ishara ya kufa pamoja na Kristo ni msalaba, je wewe unao huo msalaba katika maisha yako?
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Tofuati kati ya kifo na mauti ni ipi?
BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.
Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?
UTHAMINI WITO WA PILI WA YESU ZAIDI YA ULE WA KWANZA.
About the author