Swali: Katika kitabu cha Luka 5:1-7 tunaona kuwa Bwana Yesu aliwakuta Petro na Andrea ufukweni na akawaita, lakini tukirejea kwenye Yohana 1:35-42 tunasoma kuwa aliwaita wakati wapo kwa Yohana Mbatizaji?.. Je biblia inajichanganya?
Jibu: La! Biblia haijichanganyi hata kidogo, vinginevyo kitabu chote kitakuwa cha uongo!.. Lakini kwasababu ni kitabu cha kweli, basi kamwe hakiwezi kujichanganya!.
Kabla ya kuichambua mistari hiyo hebu tuisome kwanza..
Luka 5:1 “Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti, 2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao. 3 Akaingia katika chombo kimoja, NDICHO CHAKE SIMONI, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni. 4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki. 5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA, TUSIPATE KITU; LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU. 6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika”
Luka 5:1 “Ikawa makutano walipomsonga wakilisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa la Genesareti,
2 akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa, lakini wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.
3 Akaingia katika chombo kimoja, NDICHO CHAKE SIMONI, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.
4 Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.
5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA, TUSIPATE KITU; LAKINI KWA NENO LAKO NITAZISHUSHA NYAVU.
6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika”
Hapa ni kweli Bwana aliwakuta Andrea na Petro baharini wakivua samaki.. Lakini katika kitabu cha Yohana tunasoma habari nyingine tofauti kidogo..
Yohana 1:35 “Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. 36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! 37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? 39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. 40 ANDREA, NDUGUYE SIMONI PETRO, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. 41 HUYO AKAMWONA KWANZA SIMONI, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). 42 Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe)”.
Yohana 1:35 “Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.
36 Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!
37 Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.
38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?
39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
40 ANDREA, NDUGUYE SIMONI PETRO, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.
41 HUYO AKAMWONA KWANZA SIMONI, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).
42 Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe)”.
Uhalisia ni kwamba Bwana Yesu alikutana na Adrea na Petro kwa mara ya kwanza kipindi wanatoka kwa Yohana Mbatizaji, lakini Bwana Yesu hakuwaambia wamfuate, (yaani wawe wanafunzi wake)!.. Lakini kwa tukio lile tayari walikuwa wameshafahamiana na Bwana.
Sasa tunapokuja katika tukio la kule baharini, ndipo Kristo anawaambia waache Nyavu zao wamfuate na yeye atawafanya kuwa wavuvi wa watu badala ya kuwa wavuvi wa samaki.
Kwahiyo katika tukio hili la pili ni wazi kuwa tayari Petro na Andrea walikuwa wanamjua Bwana, Ndio maana tunaona hata haikuwa ngumu kwa Petro kumkubalia Bwana akitumie chombo chake katika kuwafundisha makutano (Na Bwana anaonyesha kama kuwa na ujasiri wote katika kutumia chombo cha Petro na kumpa maagizo kana kwamba tayari wanajuana).. na ndio maana pia tunaona haikuwa ngumu kwa Petro kumwamini Bwana na kwenda kushusha nyavu kwa neon la Bwana.. kwasababu tayari alikuwa anamjua, walishakutana huko nyuma..
Kwahiyo hakuna mkanganyiko katika habari hizo, isipokuwa ni waandishi wawili wamenukuu matukio mawili tofauti.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?
Je Bwana Yesu aliruhusu wanafunzi wake kubeba Fimbo au hakuwaruhusu? (Marko 6:8 na Mathayo 10:10).
Rudi nyumbani
Print this post
Mchungaji mimi nakaa Olmatejoo hapa Arusha.Nilikuwa nauliza huku Arusha mnapatikana kanisa lenu?
Karibu, tupo Njiro-Tanesco, wasiliana nasi kwa namba hizi 0789001312/0693036618