Elewa tafsiri ya Mithali 27:22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni.

Elewa tafsiri ya Mithali 27:22 Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni.

SWALI: Nini tafsiri ya Mithali 27:22

Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.


JIBU: Kama tunavyojua mtwangio na kinu ni vyombo vinavyotumika kuponda-ponda nafaka ngumu kuwa unga, au wakati mwingine mimea migumu kuwa milaini. Mfano wa kisamvu ambacho ili kiweze kulika, majani yake huwezi yapika hivyo hivyo huna budi kuyatwanga twanga kidogo, yalainike ndipo upike ule.

Na vivyo hivyo, nafaka kama mahindi, au ngano, ili viweze kulika zamani vilikuwa vinatwangwa kwenye vinu ,tofauti na sasa vinasagwa na mashine.

Sasa katika mithali hiyo, Mungu anatoa, asili ya mtu mpumbavu, kwamba hata akitwangwa, mfano wa ngano kinuni, huo upumbavu hauwezi kumtoka. Yaani njia gani ya lazima itumike bado hawezi kuacha upumbavu.

Sasa ni vizuri kufahamu, mpumbavu ni nani?

Mpumbavu kibiblia sio mtu Fulani mjinga tu hapana, bali ni Neno pana, linalolenga kuanzia

mtu anayesema hakuna Mungu (zaburi 14:1)

Mtu mgomvi (Mithali 9:13),

Mtenda maovu (Mithali 10:23)

Anayejiona njia yake ni sawa machoni pake (Mithali 12:15)

Mwenye kiburi (Mithali 14:3)

Mwenye dharau (Mithali 15:5)

Yaani kwa kifupi mpumbavu ni mtu ambaye hana Mungu ndani yake. Kwasababu dhambi ndani ya mtu ndio chanzo cha Upumbavu wote.

Sasa mtu kama huyu, hakuna kitu kinachoweza kuutoa upumbavu huo ndani yake, waweza kusema elimu, lakini ni watu wangapi wameelimika, lakini walevi, watukanaji, mashoga. Hata atwangwe vipi kinuni hawezi lainika, ikiwa hajui ni kipi sahihi kinachoweza kutoa upumbavu huo.

Kumfunga mwizi, hakumfanyi wizi au tamaa ya kuiba itoke ndani yake, mara ngapi unasikia mwizi katoka jela, karudia wizi wake, au ni kiongozi ambaye anaaminiwa awe kielelezo cha kupambana na ufisadi, lakini yeye ndio anakamatwa katika ufisadi, au teja ametolewa hospitalini karudia, tena madawa la kulevya. Ndio maana jamii ijapojaribu kudhibiti vitendo viovu, bado haviishi, bali hubadilika tu maumbile. Kwasababu mpumbavu hata atwangwe kinuni, hawezi geuka, hakuna nidhamu inayoweza mbadilisha. Huwezi acha mwenendo wake mbovu kwa semina za kijamii, au kuwekewa sheria

Je! Ni kipi kinachoweza kumgeuza?

Ni Yesu Kristo tu. Yeye ndiye aliyetiwa mafuta, na Mungu kuwaokoa watu wa Mungu na kuwafungua. Amwaminiye  na kudhamiria moyoni mwake kumfuata, basi atageuzwa moja kwa moja na kuwa mtu mwingine, huo ni uhakika.

Alisema.

Yohana 1:12  Bali wote waliompokea aliwapa UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.

Ni ahadi yake kuwa Ukimwamini jambo la kwanza ni kukusamehe dhambi zako, kwasababu ndio jambo lililomfanya aende msalabani kwa ajili yako miaka elfu mbili iliyopita,. Unakuwa huhesabiwi dhambi tena, unahesabiwa haki bure kwa neema yake. Lakini sambamba na hilo anakupa UWEZO wa kuwa kama yeye kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu atakayemwachia ndani yako, pindi tu unapoamini.

Na baada ya hapo utashangaa tu unavyoanza kubadilika moyoni mwako.

Zingatia tu toba ya kweli, pamoja na ubatizo sahihi (kuzamishwa katika maji mengi kwa jina la Yesu Kristo). Na kumtii yeye.

Upumbavu utakutoka.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Fahamu Maana ya Mithali 18:13 Yeye ajibuye kabla hajasikia, Ni upumbavu na aibu kwake.

HAUWEZI KURUKA MADARASA YA MUNGU!

Nini maana ya Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments