FAHAMU KANUNI ZA KUZISUBIRIA AHADI ZA MUNGU?

FAHAMU KANUNI ZA KUZISUBIRIA AHADI ZA MUNGU?

Mungu anaweza kuahidi, lakini kama hujui kanuni za kusubiria ahadi za Mungu unaweza usipokee lolote. Kila mmoja wetu amestahili kupokea lolote analo mwomba Mungu endapo ameomba sawasawa na mapenzi yake (yaani sio kwa matumizi mabaya). Yawezekana wewe umeomba Bwana akupe kazi, akupe mke/mume bora, akuponye ugonjwa wako, aikuze  karama yako n.k.

Sasa mahitaji kama hayo na mengine yoyote. Mungu alisema kwenye Neno lake, atatupatia (1Yohana 5:14). Na hivyo inakuwa kwake ni ahadi ambayo lazima aitimize. Kwahiyo wewe unachopaswa kufanya ni kusubiri tu. Kuzingojea hizo ahadi za Mungu kwasababu ni lazima zije. Jifunze tu kungojea.

Maombolezo 3:25 Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo.  26 Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu

Sasa unazingojea katika mazingira gani?. Hapo ndipo unapopaswa ujue.

Embu tuangalie kwa mtu mmoja ambaye aliahidiwa jambo na Mungu. Na hivyo alikuwa katika mazingira gani, mpaka akalipokea. Mtu mwenyewe si mwingine zaidi ya Simeoni.

Tusome.

Luka 2:25  Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, NAYE NI MTU MWENYE HAKI, MCHA MUNGU, AKIITARAJIA FARAJA YA ISRAELI; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.

26  Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.

27  Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria,

28  yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema,

29  Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema;

30  Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako,

31  Uliouweka tayari machoni pa watu wote;

Wengi wetu tukimtafakari Simeoni, tunatengeneza picha ya mtu Fulani, mzee aliyekuwa anamngoja Mungu tangu ujana wake hadi uzee atimiziwe ahadi yake. Lakini biblia haituelezi katika picha hiyo, inatueleza alikuwa ni “mtu mwenye haki mcha Mungu”. Na tazamio lake lilikuwa ni kuona mkombozi anakuja duniani, Mungu akasikia kiu yake, ndipo akamwambia utamwona.

Ni jambo gani unapaswa ujue?

Kungojea ahadi za Mungu sio tu kusema  ‘Bwana naomba hiki au kile’. Hapana, ni pamoja na kutembea katika haki na kumcha Mungu. Simoni alikuwa hivyo, hakuwa mtu anayetarajia jibu lake, huku anaendelea na udunia kama wengine, huku anaendelea ni anasa kama wanadamu  wengine, huku anaendelea ni uzinzi kama wapagani.

Alidumu muda wote, kuyalea maono aliyoonyeshwa na Mungu, katika hofu ya Kristo. Ndipo wakati ulipofika akaona alichokuwa akikitarajia.

Palilia maono yako uliyomwomba Mungu akutimizie/ au aliyokuonyesha, kwa kutembea ndani ya Kristo. Mche Mungu, kuwa mtu wa rohoni uliyejazwa Roho kama Simoni, tembea katika usafi wa Kristo, kataa udunia, na maisha ya kipagani, kuwa mwombaji.

Ni hakika hilo ulilomwomba Bwana utaliona tu, baada ya wakati Fulani, haijalishi ni gumu/zito kiasi gani, au limepitiliza muda kiasi gani. Utalipokea tu, katika ubora ambao hukuutegemea.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.

ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.

KANUNI JUU YA KANUNI.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments