Maana ya Mhubiri 10:15 Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja,

Maana ya Mhubiri 10:15 Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja,

SWALI: Je, mstari huu tunaousoma kwenye Mhubiri 10:15 una maana gani?

Mhubiri 10:15

[15]Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja, Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.


JIBU: Kwa namna ya kawaida ya kibinadamu tunajua watu wengi hutamani kuishi mijini kuliko mashambani. Kwasababu mijini huduma zote hupatikana, na ni mahali pa raha. Hata kazi, mtu anazozifanya mashambani, wengi wao ni ili matunda yake wakayafurahie mjini, Au wakaziuze bidhaa zao huko wawe matajiri.

lakini tengeneza picha mtu, ambaye anajitaabiisha kufanya kazi kwa lengo la kuzifurahia mjini, halafu hajui njia ya kufika huko, kinyume chake ndio anakwenda mbali zaidi na mji, anaelekea majangwani au mabondeni?  ni wazi kuwa mtu kama huyo  hawezi kuwa na raha katika kazi yake, kwasababu taabu yake haina faida, alikosa malengo au hakuwa na maarifa sahihi.

Ni ufunuo gani upo nyuma yake?

Na sisi pia tuliomwamini Kristo. Tuna mji ambao tunatarajia kuungia, ndio ule Yerusalemu mpya ishukayo kutoka mbinguni kwa Baba..

Ufunuo  21:2-3

[2]Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 

 [3]Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 

Anaendelea kusema…

Ufunuo  22:14-15

[14]Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. 

[15]Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

Huo ndio ule mji halisi ambao hata Ibrahimu aliona, ikamfanya aishi maisha kama ya mpitaji hapa duniani.

Waebrania 11:8-10

[8]Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 

 [9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 

 [10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. 

Umeona na sisi ili tuweze kuonekana tumestahili kuuingia katika mji huo wa mbinguni hatuna budi tuwe tumeokolewa na YESU KRISTO. Kwasababu yeye ndio NJIA ya kuuingia mji.

Ukiwa nje ya Kristo tafsiri yake wewe ni mpumbavu, kwasababu taabu yako yote ya hapa duniani, haikufikishi popote haikuepeki mjini mwa Mungu, itakuchosha tu, utakuwa na magorofa, utaijaza akaunti fedha, utakuwa ni miradi mikubwa lakini mwisho utakufa, na kwenda kaburini. Lakini ukiiona njia na kuifuata Yerusalemu basi hufanyi kazi ya bure, unapojiwekea hazina kule hufanya kazi ya kushosha, ni uzima baada ya kifo. Utafaidi matunda yake

Je umeokoka?

Ikiwa bado na unatamani kufanya hivyo, basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo >>>  KUONGOZWA SALA YA TOBA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Yerusalemu ni nini?

KWANINI KILA MWAMINI ANAPASWA AWE MHUBIRI WA INJILI

(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)Maana ya Mhubiri 1:9 “wala jambo jipya hakuna chini ya jua”. (Opens in a new browser tab)

MJI WENYE MISINGI.(Opens in a new browser tab)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments