Je ni sawa kuukubali udhaifu kama mtume Paulo alivyojisifia kwa huo? (2Wakorintho 12:9-10)

Je ni sawa kuukubali udhaifu kama mtume Paulo alivyojisifia kwa huo? (2Wakorintho 12:9-10)

SWALI: Je udhaifu ni jambo la kulikubali? Kama tunavyoona mtume Paulo akiusifia katika;

2 Wakorintho 12:9-10
[9]Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juuyangu.

[10]Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.

Paulo Hajisifii udhaufu, kana kwamba ni mzuri wa kuvutia, hapana hakuna udhaifu ulio mzuri umfanyao mtu ajiivunie huo……lakini linapokuja eneo la Mungu, udhaifu humnyenyekesha mtu, na hivyo humfanya mtu huyo kutegemea zaidi nguvu za Mungu, kuliko uweza wake mwenyewe ndicho kilichokuwa kwa Paulo.

Anasema hakuwa mtu mwenye ujuzi wa maneno, au utashi mwingi wa kitume kama wanavyodhaniwa watumishi wa Mungu wote kuwa nao.

2 Wakorintho 10:10

[10]Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu.

Lakini katika udhaifu huo wa kunena, maelfu ya watu walikuja kwa Kristo, katika udhaifu huo wa kimwili miujiza mikubwa ilifanyika kwa mikono yake. Hivyo akamshukuru Mungu kwa hilo, ili watu wasidhani ni kwa uwezo wake au kipawa chake fulani maalumu aliweza kuyafanikisha hayo.

Ndivyo tunavyojifunza hata kwa Musa, Mungu kumtumia kwa viwango vile haikuwa katika uweza wake wowote, kwasababu alikiri mbele za Mungu yeye sio mnenaji.(Kutoka 4:10), lakini pia Mungu alimshuhudia kuwa ni mpole kuliko watu wote waliokuwa duniani kipindi kile. Tofauti labda na makuhani wengine au manabii waliokuja au kuwepo kabla yake.(Hesabu 12:3)

hata leo, pale tunapojiona ni wadhaifu fulani mbele za Mungu kimaumbile au kiusemi, au kihali, hapo ndipo mahali pazuri pa kitumiwa na yeye. Usifadhaike wala usife moyo ukasema mimi siwezi, amini tu, kwasababu yeye hategemei ulichonacho, bali Neno lake moyoni mwako, ukiliweka yote yawezekana kwako. Amini tu.

1 Wakorintho 1:26-29

[26]Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;

[27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;

[28]tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; [29]mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 

fuatilia ushuhuda hizi zitakujenga..

USHUHUDA WA RICKY:

JE UDHAIFU WANGU UNAWEZA KUZUIA INJILI?

Lakini hilo halimaanishi kwamba udhaifu wowote ni mzuri, kwamba tujivunie katika hayo, hapana hakuna raha katika ulemavu, au katika ububu, au katika upofu..Lakini tujapo kwa Kristo ni mtaji mzuri wa Mungu kututumia. Hiyo ni kutudhuhirishia kuwa kwa Mungu hakuna kiungo hata kimoja ambacho hakiwezi kumtumikie yeye. Sote kwa pamoja tuwe na elimu tusiwe na elimu, tuwe na afya tusiwe na afya, tuwe na vijijini tuwe mijini, tunajukumu la kumtumikia Mungu, na kufanya vema kabisa.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.


Mafundisho mengine:

MUNGU ALIVICHAGUA VITU AMBAVYO HAVIKO.

USIMLAANI KIZIWI, WALA USITIE KWAZO MBELE YA KIPOFU.

Ipi tofuati ya “Kutakabari” na “kutakabali”?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments