NGUVU YA “KUKATAA” UNAPOPAMBANA VITA VYA KIROHO

NGUVU YA “KUKATAA” UNAPOPAMBANA VITA VYA KIROHO

Ushindi wa kwanza wa vita vya kiroho unaanza na “kukataa”.. Na kukataa kunaanza katika “moyo”, na kunaishia katika “kinywa”.. Unapoukiri udhaifu ndivyo unavyopata Nguvu juu yako vile vile unapoukiri uzima ndivyo navyo unavyopata nguvu juu yako.

Vile vile unapoukataa Udhaifu wa adui, ndivyo unavyokosa nguvu juu yako…Ndivyo biblia inavyotufundisha kuwa Uzima na Mauti vimewekwa katika uwezo wa ndimi zetu,

Mithali 18:21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake”

Ndio maana hata wokovu tunaupata kwa kanuni hiyo, Kwanza “kuamini moyoni” pili “kukiri kinywani”

Warumi 10:9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

10  Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”.

Kwahiyo daima katika maombi yako usisahau hilo kuwa “moyo na kinywa” vinashirikiana na vina nguvu..

Hivyo unapokuwa katika sala au hata nje ya sala… hakikisha siku zote unakataa moyoni mwako na katika kinywa chako Mahubiri yote ya shetani, na kazi zake anazozielekeza juu yako.

> Maana yake Unakataa “Dhambi juu ya maisha yako”.. na zenyewe zitaisha nguvu

> Unakataa “Hofu na mashaka kutoka kwa ibilisi”… na yenyewe yataisha nguvu.

> Unakataa “Unyonge na wasiwasi wa ibilisi”.. na vitaondoka katika maisha yako.

> Unakataa “Magonjwa na maradhi ya ibilisi”…. na yataisha nguvu juu yako.

> Unakataa “shida na tabu za ibilisi”.. na zenyewe zitaisha nguvu..

> Unakataa “Maazimio yote ya ibilisi yaliyokusudiwa juu yako”… na yenyewe yataisha nguvu.

> Unakataa “Maneno na ratiba zote za adui juu yako”..nazo zitafutika kabisa..

> Unakataa “kuitwa majina yote ya kiMisri uliyokuwa unaitwa huko nyuma au unayoendelea kuitwa sasa”.. na yenyewe yataisha nguvu juu yako..

Kama zamani ulikuwa kahaba, basi sasa baada ya kuokoka unakataa hayo majina, kama ulikuwa unaitwa au unajiita jambazi, au mhuni fulani au mwizi, au jina lingine lolote la kihuni na lisilo na maana unakataa hayo majina kwamaana majina nayo yamebeba roho (soma 1Samweli 25:25).

Biblia inasema Musa alipokuwa mtu mzima alikataa kuitwa Mwana wa binti Farao.. Hivyo ushindi wake wa imani ulianzia hapo..

Waebrania 11:24 “Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, AKAKATAA KUITWA MWANA WA BINTI FARAO

25  akaona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa kitambo;

26  akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.”

Kwanini Musa alikataa kuendelea kuitwa “Mwana wa binti Farao”?.. Ni kwasababu wana wa binti za Farao walikuwa wanajulikana ni watu “kuabudiwa kama miungu” pia wàtu“wenye kiburi/majivuno/majigambo” na “wauaji wenye uwezo wa kufanya jambo lolote ovu na wasiulizwe na mtu”..

Na akajua endapo akiendelea kuitwa hivyo Mwana wa binti Farao, bado hizo tabia zao zitaendelea kukaa ndani yake na kumtumikisha, hivyo akakataa hicho cheo..na kujitoa katika ile nafasi.

Inasikitisha mtu baada ya kuokoka bado anaona ni sahihi kuitwa sistaduu, au brazameni, au bishoo, au Demu, au DJ, au jina lingine lolote la kihuni tu!.. Ni lazima uyakatae hayo majina kwa kinywa chako, na pia ubadilike ili kukataa kwako kuendane na mwenendo wako.. lakini kama utakataa kinywani lakini muonekano wako unasema wewe bado ni yule yule mtu wa kale, bado itakuwa haina maana!.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.

nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

HIZO NDIZO ROHO ZA MASHETANI.

nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments