nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

nini maana ya kujikana nafsi na kujitwika msalaba?

SWALI: Bwana Yesu asifiwe. Naomba ya nifafanulie juu ya “kujikana mwenyewe” na “kujitwika msalaba” wako inamaanisha nifanye nini hasaa?


JIBU: Tusome..

Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.

35 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.

36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake”?

Kujikana ni kukataa mapenzi yako na kukubali kufuata yale ya Mungu, haijalishi yatakuwa hayakupendezi au hayakufai kwa wakati huo namna gani.

Pale ambapo, Mungu anataka ufanye hivi, na wewe unaona nafsi yako haitaki kukifanya, kwasababu moja au nyingine. sasa kule kutii cha Mungu na kukataa cha kwako huko ndiko kujikana nafsi.

Kwamfano Mungu anaposema wanawake wavae mavazi ya kujisitiri,(1Timotheo 2:9) na wewe ni mvaaji mzuri wa nguo zinazochora maungo na zile za kiume, sasa unapokubali kutii yale ya Mungu, ukaanza kuvaa magauni, bila kujali nafsi yako inakuambia utakuwa mshamba, au watu watakuambia hupendezi, huko ndiko kujikana nafsi.

Au pale Mungu anapokuambia, kiungo chako kimoja kikikukosea kikate, kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu, na kama tunavyojua kiungo ni kitu kinachojishikamanisha na wewe. Na vitu vinavyojishikamanisha na maisha yetu ni vingi, vingine vizuri, vingine vibaya, sasa pale ambapo, pengine  marafiki ulionao wanakukosesha, na kuchukua uamuzi wa kukata nao mazoea, na kuanza kutafuta marafiki wenye malengo na kimbingu na wewe, hapo ndipo umejikana nafsi.

Unapoacha, miziki ya kidunia, au kukesha kwenye muvi na kuchati  kwenye mambo yasiyokuwa na maana, na kuutumia muda huo kumtafakari Mungu, au kumtafuta yeye, huko ndiko kujikana nafsi Bwana Yesu anakokuzungumzia.

Pia Kujitwika msalaba, ni ishara ya kukubali dhiki kwa ajili ya Kristo. Kumbuka msalaba ni kitu ambacho Yesu alikibeba na kwenda kusulubishwa kwa hicho. Sio kitu ambacho alikwenda kukilalia. Ni sawa na mtu leo hii akuambie jivike mabomu yako, uende sehemu ya kujilipua.

Hivyo na sisi ili tuwe wanafunzi wa Kristo kweli, hatuna budi pia kukubali mashutumu na wakati mwingine kupitia dhiki kwa ajili ya jina lake. Hapo ndipo tutakuwa tumeonyesha tumeibeba misalaba yetu kweli kweli. Alama ya misumari yetu.

Biblia inasema..

2Timotheo 3:12 “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa”.

Wafilipi 1:29 “Maana mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, ila na kuteswa kwa ajili yake;”

Na pia Bwana Yesu alisema..

Yohana 15:20 “Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu”.

Hiyo ndio maana ya kujikana nafasi na kujitwika msalaba wako.

Bwana atujalie tuwe na moyo huo.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

YESU ANAKWENDA KUIBADILISHA OFISI YAKE.

ESTA: Mlango wa 4

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

UFUNUO NI NINI, NA NITAPOKEAJE UFUNUO KUTOKA KWA MUNGU?

PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
eto amani
6 months ago

big amen for god.

eto amani
6 months ago
Reply to  eto amani

0k

John
John
10 months ago

Nabarikiwa sana na mafundisho haya