SWALI: Ukisoma kitabu cha kumbukumbu la torati sura ya 34 unaona Musa anakufa na kitabu kinaendelea kuandika mpaka kifo chake, je huoni kuwa ni makosa kusema vitabu vitano vya kwanza vya Biblia vimeandikwa na Musa? maana mtu hawezi kuelezea kifo chake kuwa amekufa lini na kuzikwa lini?asante.
JIBU: Kuhusu uandishi wa Musa juu ya kifo chake, pia hilo linawezekana, kumbuka Musa alikuwa ni mtu ambaye alikuwa karibu sana na Mungu, hivyo Mungu kumfunulia mambo yajayo sio jambo la kushangaza sana, kama aliweza kumfunulia mambo yaliyopita, tangu Adamu, na mambo yote yaliyotendeka pale Edeni, mpaka Nuhu na Gharika yake, mpaka sodoma na Gomora, angeshindwaje kumfunulia kifo chake na kukiandika?
Lakini pia, inawezekana, waandishi wengine walimalizia kitabu hicho kwenye ile sura ya 34, kama vile Yoshua, ambaye alikuwa karibu sana na Musa, au Eleazari, ambaye alikuwa mtoto wa Haruni,mkuu wa kabila la lawi, mwingine ni Samweli, au Ezra.
Hivyo Kwa vyovyote vile, tunapaswa tujue biblia ni kitabu kilichovuviwa na Roho Mtakatifu, na hivyo yapo matukio ambayo waandishi wake tunaweza tusiwajue moja kwa moja kwasababu lengo la kitabu kile sio kuwaeleza wao, bali ni ule ujumbe uliopo ndani yake.
Hivyo cha muhimu ni Bwana azidi kutupa macho ya kuyaelewa yote yaliyoandikwa ndani yake.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
KWANINI KRISTO AFE?
TUTAMKARIBIA MUNGU KWA IDADI YA MVI ZETU ROHONI.
Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?
Biblia ina vitabu vingapi?
NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.
Rudi nyumbani
Print this post