Mungu anaketi katikati ya sifa?

Mungu anaketi katikati ya sifa?

Swali: Kwa namna gani Mungu anaketi katikati ya sifa?


Jibu: Biblia haisemi “Bwana Mungu anaketi katikati ya sifa”…bali inasema “Mungu anaketi juu ya sifa za Israeli”.

Zaburi 22:3 “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli.

4 Baba zetu walikutumaini Wewe, Walitumaini, na Wewe ukawaokoa”

Ili tuelewe vizuri ni kwa namna gani Mungu anaketi juu ya sifa za watu wake, kwanza tusome andiko lifuatalo…

Mathayo 6:10 “Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni”.

Kwa mantiki ya andiko hilo, tunona kuwa kumbe mbinguni mapenzi ya Mungu yanaendelea kufanyika, na hivyo duniani pia yanapaswa yafanyike kama yanavyofanyika huko juu…

Sasa moja ya mapenzi ya Mungu yanayofanyika mbinguni ni SIFA, ambazo MALAIKA watakatifu WANAMPA MUNGU usiku na mchana.

Na ndio maana maandiko yanasema katika 1Samweli 4:4, 2Samweli 6:2, Zaburi 80:1, Zaburi 99:1, na Isaya 37:16 kuwa Mungu ANAKETI JUU YA MAKERUBI… Na kazi ya Makerubi si nyingine Zaidi ya KUMSIFU MUNGU, na KUMPA UTUKUFU usiku na mchana, soma Ezekieli 10:18 na Ezekieli 11:22.

Na ni wapi katika biblia panapoonyesha kuwa kiti cha Enzi cha Mungu kipo juu ya makerubi, na si chini??…soma Ezekieli 1:26 na Ezekieli 10:20.

Kwahiyo kama mbinguni wanavyompa Mungu utukufu, na kwamba Mungu anaketi juu ya yao wampao sifa, hali kadhalika na duniani, Mungu anaketi juu ya sifa za watu wake! Sawasawa na hilo andiko la Zaburi 22:3.

Zaburi 22:3 “Na Wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli”.

Hivyo tunapompa Mungu sifa, basi tunakamilisha Enzi yake katikati yetu, na hivyo Mungu anashuka. Na ibada ni lazima iwe na sifa,..Sifa ni kiungo cha muhimu sana katika kuuvuta uwepo wa Mungu, na hatumsifu tu Mungu kwasababu katuambia tumsifu….Lakini tunamsifu kwasababu AMESTAHILI!!.

Kitendo cha kumtoa mwanae kwaajili yetu sisi ambao tulikuwa hatustahili, ni Dhahiri kuwa ANASTAHILI SIFA ZETU, kitendo cha kuendelea kutupa uzima na ulinzi kila siku, hakika AMESTAHILI.

Bwana atusaidie kila siku tuone sababu za kumsifu yeye.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

ANGALIA USIJE UKANG’OA NGANO KATIKATI YA MAGUGU.

KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?

NAYE ALIKUWA HANA BUDI KUPITA KATIKATI YA SAMARIA.

Sifa ni nini?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments