UMEIKUZA AHADI YAKO KULIKO JINA LAKO.

UMEIKUZA AHADI YAKO KULIKO JINA LAKO.

Jina la Bwana na Mwokozi Mkuu, YESU KRISTO libarikiwe. Karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu.

Neno la Mungu linasema…

Zaburi 138:2 “Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana UMEIKUZA AHADI YAKO, KULIKO JINA LAKO LOTE”.

Bwana anayo ahadi moja kuu aliyotuahidia, nayo ni UZIMA WA MILELE, katika YESU KRISTO.

1Yohana 2:25 “Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, YAANI, UZIMA WA MILELE”.

Hii ndio ahadi iliyo kuu ambayo Mungu katuahidia, kwamba tuwapo ndani ya mwanae YESU KRISTO, tunayo ahadi ya Uzima wa milele, (na maana ya Uzima wa Milele, ni KUISHI MILELE, Katika mbingu mpya na nchi mpya).

2Petro 3:13 “Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake”.

Sasa si kwamba Mungu hana ahadi nyingine la! Anazo tena nyingi sana!…Bwana anaweza kumpa mtu ahadi binafsi (ya kiroho au kimwili), anaweza kumwahidi mtu uzao kama alivyomhahidi Abramu, anaweza kumwahidi mtu huduma, au fursa au kitu kingine chochote, Bwana anaweza kuliahidi Taifa ahadi, au kanisa lake ahadi fulani.. (zote hizo zaweza kuwa ahadi za Mungu), na ni hakika na kweli sawasawa na 2Wakorintho 1:20.

2Wakorintho 1:20 “Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi”.

Lakini ipo “Ahadi” moja kuu ambayo KAIKUZA KULIKO ZOTE, na Zaidi sana KAIKUZA kuliko “hata jina lake”…

Zaburi 138:2b “……Kwa maana UMEIKUZA AHADI YAKO, KULIKO JINA LAKO LOTE”.

Na ahadi hiyo ni UZIMA WA MILELE.. Hii kaikuza kuliko JINA LAKE. Kwasababu tunaweza kutembea na jina lake lakini tusiwe na uzima wa milele, tunaweza kulitumia jina lake kufanya unabii, na kutoa pepo na kutenda miujiza mingi lakini tusiwe na uzima wa milele, utauliza kivipi?… tusome maandiko yafuatayo.

Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, HATUKUFANYA UNABII KWA JINA LAKO, NA KWA JINA LAKO KUTOA PEPO, NA KWA JINA LAKO KUFANYA MIUJIZA MINGI?

23  Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Umeona, kwahiyo kinachojalisha sana si jina bali ni uzima wa milele?..Je tunao uzima wa milele, au tunatembea na jina tu, na baadaye tunakuwa watu wa kukataliwa?…

Na kanuni ya kuirithi AHADI YA MUNGU (Yaani Uzima wa milele/ufalme wa Mungu) ni kwa kumwamini Bwana YESU yeye peke yake!!!!.. na kutubu dhambi kwa kumaanisha kabisa kuziacha..Baada ya hapo Roho Mtakatifu ataingia ndani na kutia alama yake ya umilele ndani yako.

Waebrania 4:1 “Basi, ikiwa IKALIKO AHADI YA KUINGIA KATIKA RAHA YAKE, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.”

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

PALE AHADI ZA MUNGU ZINAPOKUJARIBU.

FAHAMU KANUNI ZA KUZISUBIRIA AHADI ZA MUNGU?

ZIJUE TABIA ZA AHADI ZA MUNGU KWA MWAMINIO.

JINA LAKO NI LA NANI?

TUYATENDE MAMBO YOTE KWA UZURI NA UTARATIBU.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments