Yubile, wengine huiita yubilei, au yubilii.
Ni mwaka wa hamsini (50), katika kalenda ya miaka ya kiyahudi. Mungu aliwaagiza wana wa Israeli, wahesabu miaka saba, kisha waizidishe mara saba, 7×7=49.
Na ule unaofuata wa 50, uliitwa mwaka wa yubile.
Ni mwaka ambao Mungu aliwaagiza wapumzike kabisa, hawakuruhusiwa kupanda wala kuvuna. Kwa miaka miwili mfululizo(yaani mwaka wa 49 na ule wa 50), kwasababu ule wa 49 ni sabato ya kila mwaka wa 7, ndio maana miaka miwili inatokea hapo. Sasa swali la kujiuliza wangewezaje kuishi miaka yote miwili bila kufanya kazi? Jibu ni kwamba Mungu aliwabariki mara dufu katika mwaka wa 48, hivyo wakafanikiwa kukusanya vingi vya kuwatosha miaka yote hiyo miwili ijayo bila kazi.
Lakini pia ulikuwa ni mwaka wa kusamehe madeni sambamba na hilo ulikuwa mwaka pia wa kuwaachilia huru watumwa.
Walawi 25:8 Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. 9 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. 10 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. 11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa. 12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. 13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. 14 Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; 15 kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe
Walawi 25:8 Nawe utajihesabia Sabato saba za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za Sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda.
9 Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote.
10 Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu, nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake.
11 Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.
12 Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani. 13 Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake.
14 Tena kama ukimwuzia jirani yako cho chote, au kununua cho chote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe;
15 kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe
Yubile, ilifunua kazi ya msalaba baadaye. Kwani Bwana wetu Yesu ndiye aliyekuja kutimiza kazi hii rohoni.
Kwanza ndani yake tunapokea pumziko kamili la utumwa wa dhambi. Pili tunasamehewa deni zetu (dhambi zetu), Na Tatu tunafanywa huru, katika vifungo vya shetani. Yaani Magonjwa na mapepo.
Huo ndio mwaka wa Bwana uliokubaliwa, ndio Yubile yetu halisi.
lakini pia sisi kama waamini katika mwenendo wetu, tuna mambo ya kujifunza tuipatazampo Yubile?.
Kwanza ni umuhimu wa kupumzika, kuahirisha mambo yetu kupata muda na Mungu. Si tupate tu siku moja kwa wiki kuwa karibu na Mungu. Wakati mwingine Mungu anataka kipindi kirefu. Wewe kama mfanyakazi, au umejiajiri, jiwekee utaratibu baada ya kipindi fulani uwe na likizo ndefu ambayo unaitenga kwa Mungu wako,kuutafuta uso wake, ni muhimu sana.
pili tunajifunza kusamehe watu madeni yao. Si kila tunayemdai lazima atulipe, fikiria juu ya hilo. Yesu alisema achilieni nanyi mtaachiliwa. Hujui ni wapi na wewe sikumoja utakwama, na utatamani.uachiliwe.
na mwisho kuwapa uhuru watumwa wetu ikiwa wewe ni mwajiri, fikiria kuwa mfanyakazi wako anahitaji pumziko refua, mpatie, bila kumpunguzia mshahara wake. Bwana ataona umeitunza yubilee yake pia kimwili. Na sio kufanya kumbukizi ya ndoa, au kuzaliwa, hiyo sio yubilei.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!
Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?
SIKUKUU YA VIBANDA.
JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.
Rudi Nyumbani
Print this post