kiaramu ni lugha gani? je ilizungumzwa na Yesu?

kiaramu ni lugha gani? je ilizungumzwa na Yesu?

Kati ya lugha tatu ambazo zinaonekana katika uandishi wa biblia Kiaramu (Aramaic), ni mojawapo nyingine zikiwemo Kiebrania na kiyunani.

Sehemu kubwa ya agano la kale imeandikwa katika lugha ya Kiebrania na maeneo machache machache sana yalikuwa na maandishi ya kiaramu, (Ezra 4:8 – 6:18, Danieli 2: 4 – 7:28)

 Lakini katika agano jipya sehemu kubwa imeandikwa katika lugha ya kiyunani (kigiriki), na mahali pachache pachache kuna maandishi ya kiaramu.

Hivyo lugha hii haipo kwa sehemu kubwa katika biblia

Je chimbuko la hii lugha ni wapi?. 

Ni lugha iliyozungumzwa na watu walioitwa Waaramu, ambao lugha yao ilienea kwenye mataifa mbalimbali ambayo kwasasa ni nchi za Lebanoni, Syria, Yordani, Iraq, na Uturuki, na sehemu nyingine za mashariki ya kati. Ni lugha ambayo ilikuwa na nguvu sana zamani za falme zenye  kama Ashuru, na ufalme wa Uajemi. 

Enzi za Bwana wetu Yesu Kristo, lugha hii ilizungumzwa pia maeneo ya Israeli hususani katika miji ya Galilaya, ambapo Bwana wetu Yesu Kristo alilelewa. Huku kiyahudi ikiwa ni lugha ya asili, kidini na kisiasa.

Hivyo lugha kuu ya Bwana ilikuwa ni hii kiaramu, japokuwa alizungumza pia kiyahudi.

Baadhi ya maneno ya kiaramu ambayo yananukuliwa moja kwa moja kutamkwa na Bwana Yesu ni haya; (japo yapo na pia mengine)

Marko 5:41 “Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka”. 

Marko 7:34 “akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. 

Marko 15:34 “Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Maneno mengine ni kama “Hosana” (lenye maana ya okoa sasa), Mathayo 21:9

“Aba” (Marko 14:36), lenye maana ya Baba.

Lakini pia swali la kujiuliza ni nini sababu ya Bwana Yesu, kuipenyeza lugha hii katika baadhi ya matukio?

jibu ni kuwa hakuna jambo la muhimu sana katika hiyo lugha, isipokuwa ni maongozo  ya Roho Mtakatifu ndani yake kwa wakati huo. Kama tu sehemu nyingine alipoongozwa kutema mate chini atengeneze tope apake mtu machoni ili apone. 

Hivyo Bwana Yesu alikuwa ni mtu aliyetega sikio kuisikia sauti ya Roho. Vivyo hivyo na sisi, misukumo mbalimbali yaweza kuja ndani yetu. Wakati mwingine hutaomba kwa akili, utaomba kwa kunena kwa lugha, utaomba kwa nyimbo, utaomba kwa kuugua na kulia, kwa jinsi Roho atakavyokusukuma ndani.

Ni kutuonyesha kuwa Bwana hakuwa na fomula fulani pekee katika kutenda kazi, alitegemea maongozo ya Roho Mtakatifu.

Vivyo hivyo na sisi tunapojawa Roho vema. Atatugusa kwa namna mbalimbali na hivyo tutatimiza makusudio yake vizuri, katika jina lake kuu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JE! NI LAZIMA WATU WOTE WANENE KWA LUGHA?

SEMA KWA LUGHA NYINGINE.

ZIFAHAMU KARAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI KAZI WAKE.

UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments