Mwokozi wa ulimwengu (BWANA YESU KRISTO) atukuzwe.
Bwana YESU alisema katika Mathayo 7:7, maneno yafuatayo..
Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa”
Na kwanini aseme hivyo??…anaendelea mstari wa nane (8) kwa kusema..
“kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa”.
Kwahiyo kwanini tunapaswa tuombe?…jibu tumepata “kwasababu kila aombaye atapewa”… Lakini kwanini “Tutafute”..kwasababu kila “atafutaye ataona” na kwanini tubishe??… ni kwasababu “kila abishaye atafunguliwa”.
Kwahiyo matokeo ya Kuomba, Kutatufa na kubisha ni KUPEWA, KUONA, na KUFUNGULIWA.
Je unataka KUPEWA unachokitaka, na KUKIONA, na KUFUNGULIWA?...basi usikwepe mambo hayo matatu; Kuomba, kutafuta, na kubisha…usichukue moja na kuacha lingine??.. ipo sababu kwanini Bwana ayaorodheshe yote matatu.
Unataka kumjua Mungu, na kutembea katika kanuni zake? Kuwa mtu wa KUOMBA, lakini si kuomba tu bali pia na KUTAFUTA!… Unamtafutaje Mungu?, kwa kuhudhuria katika makusanyiko kila wakati kwa uaminifu, na kwa kuyasoma maneno yake usiku na mchana…na KUBISHA!..
Kubisha kunakozungumziwa hapo si “kulumbana” bali “kugonga mlango”..kwa lugha rahisi ni kitendo cha kutumia maarifa yoyote uliyonayo kufikisha ujumbe kwa aliye ndani kwamba unataka kuingia!.. Na katika kumtafuta Mungu, kubisha kwetu ni pamoja na kumtolea yeye sadaka, na kuhubiria wengine habari njema, na kufanya mambo mengine yanayofanana na hayo.
Wengi wanapenda kuomba tu na kuombewa, lakini wao wenyewe kutenga muda wa kumtafuta Mungu hawawezi.. watu wa namna hii ni ngumu sana kumpata Mungu katika maisha yao.. wanaishi kwa YESU aliyeko ndani ya mchungaji wao, au kiongozi wao (ndio maana kila kitu wanasubiri kuombewa)…lakini si hawaishi kwa YESU aliyeko ndani yao.
Hawa wataishia kuomba/ kuombewa na kupata kile wakitakacho lakini hawatamwona YESU katika maisha yao (hawataijua sauti yake wala kuongozwa na yeye)..lakini kama wangeomba na kuombewa na wangeongeza bidii katika kumtafuta MUNGU, wangepata faida zote.. kupata na kuona.
Je unaomba, na kutafuta na kubisha?
Kama hayo bado huuyafanyi basi anza kuyafanya leo, na Bwana atajifunua kwako.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.
NIFANYE NINI NIMSHINDE SHETANI?
TAFUTA KUMJUA MUNGU ZAIDI YA SHETANI
NIFANYE NINI ILI MUNGU AYAJIBU MAOMBI YANGU?
MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.
Rudi Nyumbani
Print this post