Kuota unaongea na mchungaji maana yake ni nini?

Kuota unaongea na mchungaji maana yake ni nini?

Ili kuelewa maana ya ndoto yako, jambo la kwanza ni kujiuliza ni kwanini awe mchungaji, na si mwalimu wako, au boss wako, au rafiki yako, au ndugu yako au mtu mwingine yoyote?

Ukiwaza hivyo, tendo linalofuata ni kujua kazi ya mchungaji hasa ni nini?

Mshauri:

Mchungaji ni mwakilishi wa Mungu na hivyo anafanya kazi ya kutoa mashauri bora ya kiroho kwa mafundisho sahihi (Tito 1:7-9):  Kuonyesha kuwa maisha yako yanahitaji hekima ya ki-Mungu kukuongoza, zaidi ya hekima yako mwenyewe. Kila jambo au uamuzi unaojitokeza kwenye maisha yako, mshirikishe kwanza Mungu kimaombi, kisha angalia kwenye biblia jambo hilo Mungu analiagizaje, ikiwa si rahisi kutatulika, basi ni vema ukamshirikisha kiongozi wako wa kiroho kukusaidia.

Kutoa Maonyo:

Wachungaji pia wamepewa mamlaka ya kutoa maonyo kwa kondoo wao.

2Timotheo 4:2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho

Angalia pengine katika maisha yako Mungu anakuonya / anakutahadharisha katika jambo Fulani, ambalo sio sawa unalotaka kulifanya. Hivyo zingatia sana pia hilo.

Kufariji:

Kazi ya wachungaji ni kuwalinda, kuwafariji na kuwainua waliokata tamaa. Mfano wa Yesu kristo mwokozi wetu, na faraja yetu, aliyemchungaji mkuu (Mathayo 11:28, Zab 23). Hivyo Mungu anakuonyesha kuwa yupo na wewe katika safari yako, kukuchunga, usiogope.

Lakini sababu nyingine ya mwisho (ambayo si kubwa): Yaweza kuwa ni wazo la ki-akili. Kwasababu kumbuka si ndoto zote hutoka kwa Mungu au kwa shetani, nyingine ni wazo la bongo zetu, kufuatana na mazingira yanayotuzunguka (Mhubiri 5:3). Kwamfano ikiwa mara nyingi unakuwa karibu na mchungaji wako, kuota unaongea naye mara kwa mara, itakuwa ni jambo la kawaida. Au mtu ni mpishi, kujiona yupo jikoni mara kwa mara anapika litakuwa ni jambo kawaida kabisa kwake.

Hivyo kwa ufupi ni kuwa kuota unaongea na mchungaji wako, si ndoto mbaya, bali kwa asilimia kubwa ni ya ki-Mungu. Inategemea zaidi na maudhui yake. Hakikisha tu unapiga magoti na kuomba Bwana akufunulie ni eneo lipi hasaa, ndoto yako imeegemea ukilinganisha na maisha yako, na lile eneo ambalo unaona lina uzito zaidi basi ujue hapo ndipo Mungu anasema nawe hapo. Chukua hatua.

Je! Umeokoka?

Unafahamu kuwa hizi ni siku za mwisho na Yesu amekaribia sana kurudi? Ikiwa ni la! Basi muda ndio huu, mgeukie Kristo akuoshe dhambi zako, akupe uzima wa milele bure. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo sasa, fungua hapa kwa msaada wa kuongozwa sala ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >>  KUONGOZWA SALA YA TOBA

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kuota unavua samaki, kunamaanisha nini?

Kuota unakemea mapepo/ unashindana na nguvu za giza.

Kuota unapigana na mtu.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments