Je! Tutatambuana tukifika mbinguni?

Je! Tutatambuana tukifika mbinguni?

Ndio Maandiko yanatuonyesha kuwa tutatambuana tukifika mbinguni. Ifahamike kuwa fahamu zetu au kumbukumbu zetu za hapa ulimwenguni hazitaondolewa kabisa, tufikapo mbinguni, kila pito tulipitialo, na kila jambo lililowekwa na Mungu sasa hapa duniani, lina sehemu kubwa ya fundisho la maisha yajayo. Hivyo maisha ya duniani yana thamani kama yalivyo tu maisha yatakayokuja. Ndio maana kabla ya kuingia kule ilitupaswa kwanza tupitie hapa.

Zipo sehemu kadha wa kadha katika maandiko zinatuthibitishia kuwa  tutatambuana kule mbinguni.

1). Kufufuka kwa Yesu.

Tunaona Bwana wetu Yesu Kristo alipofufuka na mwili mpya wa utukufu, aliweza kutambuliwa . Kwamfano siku ile ya kwanza ya juma Mariamu Magdalena, akiwa pale kaburini alimtambua Bwana Yesu alipozungumza naye.

Yohana 20: 16 Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu).

2) Mlima wa Mageuzi

Halikadhalika wakati ule Bwana Yesu anawachukua mitume wake watatu Petro, Yohana na Yakobo na kuwapeleka juu ya mlima ule mrefu, na kuwabadilikia sura, kama tunavyosoma watu wawili walitokea ambao ni Musa na Eliya.

Mitume waliweza kuwatambua ijapokuwa hawakuwahi  kuwaona uso kwa uso hapo kabla.

Mathayo 17:3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.

3) Fundisho la Paulo juu ya ufufuo

1Wakorintho 15:42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko

Mstari huo unatuonyesha  kuwa hatutaondolewa uhalisia wetu Tutabakia kuwa sisi sisi., isipokuwa tutavikwa utukufu wa juu zaidi. Maana yake ni kuwa tutatambuana.

4) Ahadi ya kukutanishwa tena

1Wathesalonike 4:16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana

hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.

Tutarejeshwa, na kuonana. Hivyo kwa mujibu wa vifungu hivyo katika ulimwengu ujao sote tutajuana na kufahamiana.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest


0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments