Jibu: Turejee..
Kumbukumbu 28:13 “Bwana atakufanya kuwa KICHWA, WALA SI MKIA; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;
14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia”.
Unaweza kutafakari kwanini hajasema Utakuwa KICHWA na wala si MGUU!.. kwasababu kichwa kipo juu na miguu ipo chini, na ndio sehemu ya mwisho ya mwili wa mtu… lakini badala yake anasema Utakuwa “kichwa”na si ”mkia”. Je kuna sifa gani mbaya katika mkia?
Sasa sote tunajua kuwa mwanadamu hajaumbwa na Mkia, bali kichwa tu peke yake, hivyo bila shaka hapo biblia imejaribu kutumia umbile la wanyama badala ya la mtu kufunua hali ya mtu atakayemcha MUNGU na yule ambaye hatataka kumcha MUNGU, kwasababu wanyama ndio wenye kichwa na mkia na si mwanadamu.
Sasa kichwa cha mnyama yoyote ndicho kinachoongoza mwili wote, na ndio sehemu ya kwanza ya mwili wa mnyama. Lakini Mkia ni sehemu ya mwisho kabisa ya mwili wa mnyama, na sehemu hii imeungana na sehemu ya haja kubwa ya mnyama. Kwahiyo wakati kichwa kinapokea chakula fresh, mkia unapokea uchafu (kinyesi).
Ikiwa na maana kuwa watu wanaomcha MUNGU, watapokea vilivyo visafi na vya kwanza na vizuri, na wasiomcha MUNGU ni kinyume chake, watapokea vile vya mwisho na visivyo na heshima vilivyo haribika.
Pia watu wanaomcha MUNGU watakuwa wa kwanza, kulingana na sifa ya kichwa, lakini wasiomcha MUNGU watakuwa wa mwisho kama ilivyo nafasi ya mkia katika mwili wa mnyama, sasa hebu tafakari unakuwa wa mwisho na bado unapokea vilivyo vichafu (mfano wa vinyesi)..ni jambo baya sana..
Ni tahadhari kwetu tunaoishi, kwamba tuwekeze nguvu kubwa katika kumtafuta MUNGU ikiwa tutataka tuwe vichwa, lakini tusipotaka kufanya hivyo, maandiko yanasema tutakuwa mkia na maadui zetu MUNGU atawaweka juu yetu na sisi tutakuwa wa mwisho.
Kumbukumbu 28:43 “Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.
44 Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; YEYE ATAKUWA NI KICHWA, WEWE UTAKUWA MKIA.
45 Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza”
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MAUTI NA UZIMA HUWA KATIKA UWEZO WA ULIMI.
AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.
NI SAHIHI KABISA, HUU SI WAKATI WA TINI!
Maana ya Mafarisayo Hupanua HIRIZI zao, na kuongeza MATAMVUA yao
About the author