Shalom,
Je unajua Pepeto ni nini na kazi yake ni ipi?
Turejee Mathayo 3:11-12.
Mathayo 3:11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
12 Ambaye PEPETO LAKE li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya NGANO yake ghalani, bali MAKAPI atayateketeza kwa moto usiozimika”.
Pepeto ni kifaa maalumu chenye umbile kama la “UMA” ambacho wakulima wa nafaka kama ngano, wanakitumia kupuria/kupepetea ngano.. sasa jamii zetu zinatumia NYUNGO kupepetea nafaka kama mchele na ngano, ambapo ungo ule unazurusha juu nafaka kisha upepo unatenga ile nafaka na makapi.
Lakini zamani wakulima wa ngano hawakutumia nyungo, kwani kulikuwa na matita mengi ya ngano, hivyo UNGO usingetosha kuimaliza kazi yote, hivyo walitumia kifaa hiko kinachoitwa Pepeto, ambacho kinafanana sana na UMA. (Tazama picha chini).
Sasa kiroho Ngano ni “NENO LA MUNGU”, na makapi ni “NDOTO NA MAONO YA UONGO” katika siku za mwisho Bwana atatenga Neno lake na maono ya uongo, na watu wanaolifuata Neno lake na wanaofuata manabii wa uongo.
Yeremia 23:25 “Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu, wakisema, Nimeota ndoto; nimeota ndoto.
26 Je! Mambo hayo yatakuwa katika mioyo ya manabii wanaotabiri uongo hata lini, manabii hao wenye udanganyifu katika mioyo yao wenyewe?
27 Wanaodhania ya kuwa watawasahaulisha watu wangu jina langu kwa ndoto zao, wanazomhadithia kila mtu jirani yake, kama vile baba zao walivyolisahau jina langu, kwa ajili ya Baali.
28 Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye ALIYE NA NENO LANGU, na aseme neno langu kwa uaminifu. MAKAPI NI KITU GANI KULIKO NGANO? Asema Bwana”.
Mstari wa mwisho hapo anasema, “Makapi ni kitu gani kuliko Ngano” ikimaanisha kuwa makapi ni unabii/ndoto za uongo zinazotolewa na manabii wa uongo si kitu mbele ya Neno la MUNGU linalofananishwa na Ngano.
Kwahiyo katika siku za mwisho, YESU KRISTO ambaye ndiye pepeto lenyewe, atatenga makapi na ngano, na wanaotumainia makapi na wale wanalotumainia Neno lake.
Hizi si siku za kupelekwa huku na kule na manabii wa uongo, wanaoshinda kutwa kuchwa kutabiri maono ya uongo, wakiwaaminisha na kuwatumainisha watu katika vitu vya ulimwengu huu, kwamba kuwa na hivyo ndio kielelezo cha kwanza cha kukubaliwa na MUNGU.
Bwana YESU alisema, itamfaidia nini mtu apate ulimwengu mzima na kisha apate hasara ya nafsi yake (Marko 8:36)?..maana yake utabiriwe na nabii au mchungaji au mtume kwamba utapata hiki na kile cha ulimwengu huu, na wakati huo huo haioni dhambi maishani mwako, je hayo aliyokutabiria yatakufaidia nini ikiwa utapoteza uzima wa milele?
Hizi ni siku za mwisho na pepeto hili limeshaanza kupita, na Roho Mtakatifu anawatenga walio wa kwake, hatua hizo zikimalizika kinachofuata ni unyakuo wa kanisa, ambapo walioishi na kulifuata Neno la MUNGU watakusanywa ghalani (mbinguni).. lakini waliofuata makapi watatupwa katika lile ziwa la moto, ndivyo maandiko yanavyosema..
Mathayo 13:29 “Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.
30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu…
40 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.
41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MAMBO SITA, AMBAYO MUNGU HUTUMIA KUONDOA UOVU NDANI YA MTU.
Ipi tofauti kati ya Uhai na Uzima kibiblia?
KIMBIA MACHAFU YA DUNIA. (2Petro 2:20)
Je kibiblia ni sahihi kuadhimisha jumapili ya mitende?
“Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama
About the author