KIMBIA MACHAFU YA DUNIA. (2Petro 2:20)

KIMBIA MACHAFU YA DUNIA. (2Petro 2:20)

2 Petro 2:20 “Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia MACHAFU YA DUNIA kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza”. 

Mstari huo unatupa uelewa kwamba kumbe tukimjua mwokozi wetu Yesu Kristo, ni lazima kuambatane na kuyakimbia machafu ya dunia. Haiwezekani mtu akamjua Yesu Kristo halafu asiyakimbie Machafu ya dunia Kwa mujibu wa huo Mstari.

Machafu ya dunia ni yapi?

Machafu ya dunia ni Yale mambo maovu uliyokuwa unayafanya ulipokuwa mwenye dhambi, mfano ulevi, uzinzi, wizi, ushirikina, anasa, utoaji mimba, ulawiti,  n.k.

Sasa ikiwa ukinaswa, na kushindwa kutoka huko, maandiko yanasema hali yako ya mwisho inakuwa mbaya kuliko Ile ya kwanza, maana yake kama ulikuwa ni mgonjwa kidogo, kutokana na madhara uliyoyapata katika Ile dhambi, basi ugonjwa unakuwa mara dufu zaidi, kama ulikuwa unaweza kujizuia usilewe mara Kwa mara, basi nguvu ya ulevi inakulemea mara mbili unakuwa mlevi yule wa kupindukia kabisa kabisa.. hiyo ni kutuonyesha ni jinsi gani tunapaswa tuwe makini kama vile maandiko yanavyosema  pindi tuokokapo tuutimize wokovu wetu Kwa kuogopa na kutetemeka.

Wafilipi 2:12  “Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka”.

Bwana Yesu alitumia mfano wa Yule mtu ambaye alikuwa na pepo, lakini alipomtoka hakujiweka sawa, matokeo yake ikawa ni Yule pepo kuchukua pepo wengine saba waovu kuliko yeye, na hali yake ya mwisho ikawa mbaya kuliko ile ya kwanza. (Mathayo 12:43)

Lakini ikitokea tayari umeshaanguka kwenye machafu ya dunia, ambayo uliyaacha huko nyuma. Je ufanyaje?

Ni kutubu haraka sana. Angali nafasi unayo. Kumbuka hapo anasema “akinaswa na kushindwa”

Maana yake ni kuwa kama umenaswa, ni kufanya hima ujinasue kabla mwindaji wako (ibilisi), hajakuweka mikononi mwako kabisa kabisa. Lakini ukishindwa.basi Ndio mwisho wako umefika.

Ikiwa ulirudia uzinzi, ulirudia ulevi, ulirudia anasa, ulirudia kujichua, kutazama picha chafu mitandaoni.. Acha haraka sana, toka huko kwa kasi zote, jitakase kwa Bwana, kisha maanisha kumfuata Yesu, huku ukiutimiza wokovu wako kwa kuogopa na kutetemeka, kwasababu huo tumekabidhiwa mara moja tu.

Na Bwana atakurehemu.

Bwana akubariki.

Ikiwa bado hujaokoka na utapenda leo kumpokea Kristo maishani mwako. Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Wokovu wa milele/ Ulinzi wa daima (eternal security) Je! ni neno la kimaandiko?

MFALME ANAKUJA.

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)

JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

TABIA ZITAKAZOMTAMBULISHA MPINGA-KRISTO AJAYE.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments