Mithali 1:20 Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja; 21 Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake.
Kibiblia, hekima, ni uwezo wa kupambanua , kuhukumu na kufanya maamuzi yenye matokeo makamilifu ya Ki-Mungu duniani.
Kwamfano, biblia inatuambia kwa hekima Mungu aliziumba mbingu na nchi (Mithali 8:22-31)
Sulemani alimwomba Mungu hekima ya kuchunga na kufanya hukumu kwa watu wake Israeli, na Mungu akampa, Danieli alipewa hekima ya upambanuzi wa ndoto na maono yote ya siri,
Kwa ufupi hekima ya ki-Mungu ni zaidi ya maarifa, elimu, au akili, ni uwezo wa juu sana ambao unazidi upeo wa ki-binadamu.
Kumbuka Biblia inaitaja hekima pia kuwa ni mtu. Na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO.
1Wakorintho 1:24 bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.
Na kama Ndio hekima mwenyewe..Basi ndani yake matunda yote ya hekima yapo.
Wakolosaia 2:3 ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.
Hivyo ili mtu kuiona hekima tafsiri yake ni kuwa anapaswa amwone YESU. Na kumwona Yesu ni kumpokea kama Bwana na mwokozi wa maisha yako (Warumi 10:9), pamoja na kumtii kutembea katika njia zake.
Katika mahubiri, Mahubiri yanapatikana wapi? Kila mahali, kwenye njia kuu, viwanja, kwenye mikutaniko ya watu, mastendi, masokoni, mitandaoni n.k.
Anapazaje sauti?
Anapaza sauti kupitia watumishi wake mbalimbali Aliowatuma kumuhubiri.
Hivyo, hilo andiko linalosema,
Mithali 1:20 Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja; 21 Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake.
Unaweza kuelewa sasa analenga injili, inayohubiriwa kila mahali duniani kote. Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayeweza kusema hajawahi kuisikia injili, kwasababu kila mahali inahubiriwa kwa nguvu. Kuonyesha kuwa hekima haijajificha ipo sikuzote, bali ni watu ndio wanaikwepa.
Mtu yeyote anayemwamini Kristo basi tayari amefungua mlango wa ufahamu mkubwa sana unaoweza kufungua mambo yote katika hii dunia.
Bwana akubariki.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
About the author