Fahamu maana ya Warumi 7:25 je tunatumikia sheria ya dhambi?

Fahamu maana ya Warumi 7:25 je tunatumikia sheria ya dhambi?

SWALI: Naomba kufahamu Warumi 7:25 ina maana gani?

Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.

JIBU: Katika sura yote ya saba, mtume Paulo, anaeleza kwa kina mapambano yaliyo ndani ya mwamini.  Kwamba nia yake kutoka ndani ni kuitii sheria ya Mungu, lakini mwili wake kwa nje ni kikwazo kikubwa kiasi cha kumfanya ashindwe kabisa kutimiza maadhimio yake.

Warumi 7:19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu

Na ni kweli huo ndio uhalisia wa kila mtu. Na ndio maana mwishoni mwa sura hiyo anahitimisha kwa kueleza hali hiyo, Lakini katika vifungu hivyo, wengi wanatafsiri vibaya wakidhani  Paulo anatetea udhaifu wa mwili hapana.. Kinyume chake alianza kwanza kueleza uhalisia wa kibinadamu, ili atoe suluhisho halisi la namna ya kushinda, ambalo ndio tunalisoma katika sura inayofuata ya nane (8)

Ambapo sasa kwenye sura ya nane(8) inayofuata, anaeleza namna ambayo Kristo anatusaidia kuishinda hiyo hali, kwa sheria nyingine  mpya ya Roho ambayo anaiweka ndani yetu.

Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Maana yake ni kuwa, Roho Mtakatifu, anatuweka huru katika huo utumwa wa mwili unaotupelekesha.

Inahitaji tu kutii, kwa kumfuata Roho Mtakatifu, kisha yeye mwenyewe atatupa nguvu ya kushinda mambo yote ya mwilini. Lakini sio kwa kutegemea  nguvu zetu tu wenyewe.

Warumi 8: 5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.

7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.

10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.

Hivyo ukiishi kwa kumtii Roho Mtakatifu, basi huwezi tumikishwa tena na  mwili,

Wagalatia 5:16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.

17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

Hitimisho:

Warumi 7:25, Paulo analenga hasaa sababu ya sisi kushindwa kutimiza sheria ya Mungu, Ni kwasababu ipo sheria nyingine (ya dhambi iliyojificha ndani yetu) ambayo ni ngumu kutoka kwa namna ya kibinadamu, hivyo anataka hilo tulijue ili tufahamu kuwa kwa nguvu zetu wenyewe hatuwezi kuishinda, Lakini kwa Yesu Kristo atupaye Roho wake ndani yetu, tukienenda kwa kumtii huyo, basi sheria hiyo ya dhambi tutaishinda kabisa kabisa.

Ni wito wa kila mwamini kujifunza kutembea katika Roho.

Je! Unafahamu namna ya kutembea katika Roho kama sio. Basi tutumie ujumbe kwa namba uzionazo chini ya somo hili tukutumie.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?

MAANA ROHO HUCHUNGUZA YOTE, HATA MAFUMBO YA MUNGU.

Print this post

About the author

Devis administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments